Cameroon
ni taifa lililopo katika ukanda wa Afrika ya Kati, wakati mwingine huelezwa
kuwa lipo katika Ghuba ya Guinea.
Limepakana na Nigera kwa upande wa Magharibi
na Kaskazini, Chad kwa upande wa Kaskazini Mashariki, Jamhuri ya Afrika ya Kati
kwa upande wa Mashariki, Guinea ya Ikweta, Gabon, na Jamhuri ya Congo au
Congo-Brazzaville kwa upande wa Kusini.
Mwambao wa pwani wa taifa hilo upo
katika ukanda wa Bight of Biafra, Ghuba ya Guinea na Bahari ya Atlantiki.
Japokuwa taifa hilo sio mwanachama wa nchini za Afrika Magharibi ECOWAS lakini
kwa kiasi kikubwa kijiografia imetoa mchango mkubwa katika historia ya ukanda
huo.
Wakati mwingine taifa hilo huwa linachukuliwa kama ni taifa lililopo
katika ukanda wa Afrika Magharibi kuliko Afrika ya Kati.
Taifa hilo lina zaidi
ya lugha za kienyeji 250 zinazozungumzwa na takribani watu milioni 20. Kuitwa
Cameroon kulitokana na ujio wa Wareno katika karne ya 15 waliofika pwani ambapo
walipaita Rio dos Camarões (Yaani mto
Shrimp) ambapo baadaye waingereza wakaliita eneo hilo Cameroon.
Ustarabu wa
Jamii za Sao uliopo pembezoni mwa Ziwa Chad na ule wa Baka uliokuwa ukiishi
katika misiti iliyopo Kusini Mashariki ulilifanya eneo hilo kuwa maarufu. Jamii
ya Sao walikuwa wavuvi wakati Jamii ya Baka walikuwa wawindaji.
Mnamo
mwaka 1884 Wajerumani walichukua mamlaka ya kulikalia eneo hilo ambapo nao
wakawa wanaliita Kamerun.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Ufaransa na
Uingereza ziligawiwa eneo hilo chini ya League of Nations. Mapema miaka 1950harakati
za kutaka uhuru wake kwa tiketi ya UPC kulileta vita kali ya Bamileke baina ya
Wafaransa na UPC ambayo iliendelea tena hadi mapema miaka 1971.
Mnamo mwaka
1960 Ufaransa ilinyosha mikono na kuachia ambapo mzawa wa Cameroon Ahmadou
Ahidjo. Upande wa Kusini haukukubaliana na uhuru huo hadi ilipofika mwaka 1961.
Serikali ya Shirikisho ilivunjwa mnamo mwaka 1972.
Taifa hilo lilianza uitwa
Jamhuri ya Muungano wa Cameroon na sehemu nyingine iliendelea kutumia Jamhuri ya Cameroon. Wakazi wengi wa taifa
hilo ni Wakulima wa taifa hilo wanachukua iadadi kubwa ya watu nchini humo. Rais
wa sasa wa taifa hilo ni Paul Biya liyeliongoza tangu mwaka 1982.
Tangu mwaka
2017 kumekuwa na mgogoro baina ya jamii ya watu wanaozungumza Kiingereza
waliopo Kusini wakitaka kujitenga. Kiingereza na Kifaransa ndio lugha
zinazotumika katika taifa hilo. Taifa hilo lina mlima mrefu kuliko yote nchini
humo wa Mount Cameroon wenye futi 13,500.
Mji mkuu wa taifa hilo ni Yaounde.
Mji mkuu wa pili kwa ukubwa ni Douala. Taifa hilo limekuwa maarufu kutokana na
aina ya muziki wa asili wa taifa hilo wa Makossa na Bikutsi.
Na pia limekuwa
maarufu kutokana na maendeleo makubwa ya soka ambayo yalitokana na timu ya
taifa hilo maarufu ‘Simba Wasioshindika’ au ‘Indomitable Lions’. Cameroon ina
ukubwa wa kilometa za mraba 475,442 linalokaliwa na takribani watu milioni 25.
Imetayarishwa
na Jabir Johnson……………………………….Novemba 20, 2019.
0 Comments:
Post a Comment