Friday, November 8, 2019

Sudan ni taifa la namna gani?

Sudan ni taifa lenye takribani watu milioni 43 ambalo linapakana na Misri kwa upande wa Kaskazini, Bahari ya Shamu kwa upande wa Kaskazini Mashariki.

Pia linapakana na Sudan Kusini kwa upande wa Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa upande wa Kusini Magharibi, Chad kwa upande wa Magharibi na Libya kwa upande wa Kaskazini Magharibi. 

Taifa hilo lina ukubwa wa kilometa za mraba 1,886,068 hivyo kulifanya kuwa taifa la tatu kwa ukubwa barani Afrika. Dini ambayo imetamalaki katika radhi hiyo ya Sudan ni Uislamu. 

Lugha zinazozungumzwa katika taifa hilo ni Kiarabu na Kiingereza. Mji mkuu wa taifa hilo ni Khartoum. 

Mji huo upo kati ya maungio ya mto Nile ya Bluu na Nile Nyeupe. Tangu mwaka 2011, taifa hili liliingia katika mgogoro wa kijeshi kutokana na mikoa ya Kordofan ya Kusini na Nile ya Bluu. 

Baada ya utawala wa kiimla katika eneo hilo; ndipo katika karne ya 20 kuliposhuhudiwa mapambano ya kutaka Sudan na mnamo mwaka 1953 Waingereza waliipa haki zote za kujitawala. Ilipata uhuru wake Januari 1, 1956. 

Tangu kupata kwa uhuru kwa taifa hilo Sudan imekuwa na serikali zisizofuata misingi ya demokrasia ikiwamo mapinduzi ya kijeshi. Itakumbukwa chini ya utawa wa Gaafar Nimeiry , Sudan ilikuwa chini ya sheria za kiislamu zilizotungwa mwaka 1983. 

Hatua hiyo ililiffanya taifa hilo ligawanyike watu wa kaskazini walio wengi ni waislamu na kusini ni waumini wa dini ya kikristo hali iliyozaa kutoelewana. 

Pia imeshuhudiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hili tofauti katika lugha, dini na mamlaka ya kisiasa vikiibuka na kulitafuna kabisa. 

Utawala wa kibabe wa miongo mitatu ya Omar al-Bashir kutoka mwaka 1989 hadi 2019 ulishuhudia mgawanyiko wa taifa hilo hadi kuzaa taifa jingine la Sudan Kusini. Mgogoro wa kivita katika Jimbo la Darfur uliolipuka mwaka 2003 umesababisha watu akali ya 400,000 kupoteza maisha. 

Maandamano ya umma ya mwaka 2018 yalihitimisha safari ya Mbabe Omar al-Bashir aliyelazimika kujiuzulu Aprili 11, 2019. Katika suala la mazingira jangwa ndio limechukua sehemu kubwa ya Sudan hivyo mmomonyoko wa udongo na ukosefu rutuba katika udongo. 

Mvua zimekuwa zikinyesha kuelekea Kusini katika ya Juni na Septemba. Upande wa kaskazini umekuwa ni ukikaliwa na Jangwa la Nubia. 

0 Comments:

Post a Comment