Mwenyekiti wa Chama cha
NCCR- Mageuzi Taifa na Mbunge wa Vunjo mkoani Kilimanjaro James Mbatia amekutana na wagombea uchaguzi wa Vijiji na
Vitongoji na kupitisha maazimio baada ya kujitoa katika kinyang’anyiro cha
uchaguzi wa serikali za mitaa wa Novemba 24, 2019.
Maazimio hayo yamefikiwa Novemba
23, 2019 katika mkutano na waliokuwa wagombea wa chama hicho katika ngazi ya
vijiji na vitongoji katika Jimbo la Vunjo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kwa Njovu, Himo.
1.
Kwa
kuwa TAMISEMI wana mgongano wa maslahi katika kusimamia uchaguzi huu, chama cha
NCCR-Mageuzi kinashauri kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo haitashirikisha
watendaji wa kat wala vijiji, wakurugenzi na vyombo vingine vya dola. Uchaguzi
usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.
2.
Kamati za Maendeleo za kila kijiji ziundwe
na viongozi wetu ambao walinyimwa fursa ya kugombea na Chama cha Mapinduzi, ili
maendeleo ya wananchi yaendelee mbele. Na hii ni kwasababu wanaosemekana kuwa
ni viongozi waliopiya bila kupingwa baadhi yao ni wahalifu, walevi wa kupindukia,
wengine ni wagonjwa wa akili na wasio na maadili wala hawana uwezo wa
kuiunganisha jamii.
3.
Kwa
kuwa Chama cha Mapinduzi na serikali yake imetubagua na kutunyima haki ya
kidemokrasi ya kuchagua viongozi wetu
Chama cha NCCR-Mageuzi kinatoa siku 30 za kupata majawabu ya mchakato
mzima. Na serikali serikali haitatoa majawabu Chama chetu hakitatoa ushirikiano
kwa viongozi walioteuliwa na CCM katika Jimbo la Vunjo.
4.
Kwa kuwa mchakato mzima wa uandikishwaji wa wapiga kura hadi uchukuaji wa fomu ulikiuka kanuni na mwongozo wa uchaguzina
kutumia pesa za wananchi kuendesha mchakato huo
ambao umegubikwa na ulaghai wa matumizi ya pesa na kusababisha hisia za
utakatishaji wa fedha hivyo Chama cha NCCR-Mageuzi ngazi husika kione jinsi ya
kuwasiliana na Wanasheria, Taasisi za haki za bibnadamu na Taasisi mbalimbali
za Kimataifa kuingilia kati suala hili la ukiukwaji wa Haki za Msingi za
Binadamu.
5.
Kwa kuwa viongozi wa serikali za mitaa,
vijiji na vitongoji wanafanya kazi kwa kujitolea na kushirikiana na jamii
husika katika kuleta maendeleo ya eneo husika hivyo basi upatikanaji wa
viongozi utokane na jamii husika bila kudhamiwa na vyama vya siasa na
kutojihusisha juu ya mchakato mzima wa kupata viongozi hawa.
6.
Chama cha NCCR-Mageuzi kinashauri kuharakisha
upatikanaji wa Katiba Mpya itakayowaongoza watanzania na serikali ya Tanzania.
0 Comments:
Post a Comment