Taifa
hili lipo Afrika Magharibi ambapo lilianza kutumia jina hilo kutokana na jina
la mto Niger. Linapakana na Libya kwa upande wa Kaskazini Mashariki, Chad kwa
upande wa Mashariki, Nigeria kwa upande wa Kusini, Benin kwa upande wa Kusini
Magharibi, Burkina Faso na Mali kwa upande wa Magharibi na Algeria kwa upande
wa Kaskazini Magharibi.
Taifa hilo lina ukubwa wa kilometa za mraba 1,270,000
hivyo kuwa miongoni mwa mataifa makubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Zaidi ya asilimia 80 ya ardhi ya taifa hili imekaliwa na Jangwa la Sahara.
Pia
Niger ni taifa ambalo lina waislamu kwa kiasi kikubwa kwa takribani ya waamini
milioni 22 wa dini hiyo.
Aidha waamini walio wengi wanaishi katika makundi
makundi Kusini na Magharibi mwa Niger. Mji mkuu wa Niger ni Niamey ambao upo
pembezoni mwa taifa hilo kwa upande wa Kusini Magharibi.
Kwa mujibu wa takwimu
za Umoja wa Mataifa taifa la Niger linashika nafasi ya 189 kati ya 189 katika
kile kinachofahamika kama Human Development Index (HDI).
Maeneo ambayo sio ya
jangwa katika taifa hilo la Niger yamekuwa yakikabiliwa na ukame. Uchumi wa
taifa hili umekuwa chini zaidi ukitegemea kilimo katika maeneo machache yenye
rutuba.
Hali hiyo imekuwa ikiliongezea gharama kubwa taifa hilo kutokana na
kuongezeka ka kasi kwa idadi ya watu. Licha ya changamoto lukuki katika taifa
hilo ikiwa elimu duni, umasikini kwa watu wake.
Miundo mbinu mibovu uchumi wa
taifa umekuwa ukitegemea madini ya Uranium. Taifa la Nigerlimekuwa likikabiliwa na vikwazo
kutoka mataifa makubwa. Kisiasa taifa hilo limeishi katika vipindi vitatu vya
utawala wa kijeshi na mabadilikio mara tano ya katiba.
Kwa sasa bado
inashikilia mfumo wa vyama vingi huku idadi kubwa ya watu ikiisha zaidi
vijijini kuliko mjini. Niger iliingia katika mfumo wa vyama vingi baada ya
mapinduzi ya kijeshi mwaka 2010.
Rais wa sasa wa taifa hilo linalozungumza Kifaransa
ni Mahamadou Issoufou aliyeingia madarakani tangu Aprili 2011.
Imetayarishwa na Jabir Johnson………………Novemba
19, 2019
0 Comments:
Post a Comment