Waziri wa Mambo ya Kigeni
wa Misri Sameh Shoukry amejibu kauli ya Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan
kuwa hali ya uchumi iliyopo nchini humo sio sawa na ile ya Uturuki.
Katika siku
za hivi karibuni Erdogan alikaririwa akisema kuwa Uturuki ilivyo kwa sasa kiuchumi
sio kama Misri. Katika mahojiano kwa
njia ya simu na mtangazo wa kituo cha televisheni cha MBC Amr Adib jana
jumapili Shoukry alisema tuhuma za
kwamba uchumi wa Misri unashuka ni taarifa za kuchekesha.
Waziri huyo wa mambo
ya kigeni aliongeza kuwa Misri ina miradi kadhaa ya kitaifa, pia kuna ripoti
chanya za kimataifa kuhusu uchumi wake, pia kushuka kwa dola ya Marekani
kunathibitisha madai ya Erdogan sio sahihi.
Pia Shoukry alisema asilimia 8 ya
watu imepata ajira nchini Misri hivyo kupunguza pengo la wasio na ajira katika
taifa hilo na uchumi wa Misri kukukua kwa asilimia 5.8 ni alama chanya za
kiuchumi.
Julai 15, 2016 Erdogan alinusurika katika jaribio lililoshindwa la
kumtoa madarakani lakini pia alipokea vitisho kutoka nje na kwamba Uturuki iliyapokea machafuko ya
hivi karibuni katika nchi za Syria, Misri na Libya kwa sura tofauti.
Hata hivyo
hiyo sio mara ya kwanza kwami miaka mitano iliyopita kumekuwa na kurushiana
maneno kwa maofisa wa Misri na Uturuki pamoja na baadhi ya vyombo vya habari
hususani baada ya kung’olewa madarakani kwa Rais wa zamani wa Misri Mohamed
Morsi Julai 3, 2013.
CHANZO: EGYPT INDEPENDENT
0 Comments:
Post a Comment