Waziri Mkuu wa Eritrea Abiy Ahmed |
Waziri Mkuu wa Eritrea
Abiya Ahmed ameyapinga maneno ya wakosoaji wake kuwa serikali yake ni dhaifu na
iliyojaa woga kutokana na idadi ya watu waliokufa katika maandamano ya kumtaka
aachie ngazi ikifikia 86.
Maandamano hayo yalianza
Oktoba 23 yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 80 huku Abiy akikosolewa kwa
kuwa na mwendo wa kinyonga katika utatuzi wa vurugu hizi.
Juzi Jumapili Abiy
akizungumza kupitia kituo cha televisheni alisema haoni sababu ya kutumia nguvu
kuzuia vurugu hizo isipokuwa majadiliano ya pamoja na serikali ya Ethiopia
kuhusu vurugu hizo zilianzia mjini Addis Ababa na baadaye katika mkoa wa Oromia
nchini Ethiopia.
Mshindi huyo wa tuzo ya
Amani ya Nobel ambaye alichukua madaraka ya kuliongoza taifa hilo mwaka
uliopita amesema amechagua majadiliano katika meza ya pamoja na elimu badala ya
kutumia nguvu.
Hata hivyo aliwataka wote
wanaofikiri uvumilivu wake ni tafsiri ya udhaifu na woga waachane na hoja hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi Billene Seyoum alitangaza wiki iliyopita kuwa vifo
vilikuwa 78 na 76 miongoni mwao walipoteza maisha kutokana na msongamano kwenye
vurugu hizo.
Abiy aliongeza kuwa 10 kati
yao waliuawa kutokana na kupambana ana kwa ana na vyombo vya ulinzi na usalama.
Wengi wa waliopoteza maisha katika vurugu hizo ni wa kabila la Oromo
wakifuatiwa na Amhara.
Waziri Mkuu huyo anatokea
kabila la Oromo na vurugu hizo zinakuja nchini humo wakati uchaguzi mkuu
ukitarajiwa kufanya Mei 2020.
CHANZO: TesfaNews
0 Comments:
Post a Comment