Misri ya sasa ina historia
ndefu mno kwani miaka 3100 iliyopita kulitokea muunganiko wa Misri ya Juu
(Ta-Shome) na Misri ya Chini (Ta-Mehu) na kupata Misri moja.
Hivyo kupitia
historia hiyo ya muungano, inaelezwa kuwa kuwa Misri ilikuwa na mgawanyiko wa kijiografia.
Pia katika taifa hilo kumekuwa na mgawanyiko ambao umewekwa katika vipindi
tofauti vitatu.
Misri ya Zamani (Old Kingdom of Egypt), Misri ya Kati (Middle
Kingdom of Egypt) na Misri ya Mpya (New kingdom of Egypt). Misri ya Zamani ni
kile kipindi ambacho Misri ilijiwekea historia yake kuanzia miaka ya 2700-2160
K.K
Kwa upande wa wanaakiolojia huita Misri ya Zamani kuwa kipindi cha ujenzi
wa Mapiramidi kwa ajili ya makaburi ya Mafarao wa wakati huo. Katika kipindi
cha Misri ya Kati, ni kile kipindi kati ya mwaka 2023-1633 K.K
Na upande wa
Misri Mpya ni kile kipindi kuanzia miaka ya 1550-1070 K.K
Kwa wanaakiolojia
huita kipindi hiki kama kipindi cha kupanuka, yaani Wamisri waliweza kusambaa
sehemu mbalimbali dunia kwa malengo ya kukuza ustaarabu.
Suala hili
linajidhihirisha kwenye ushahidi wa uwepo kwa Waafrika barani Amerika kabla ya
Wazungu. Maana kule Amerika ya Kusini kuligunduliwa Piramidi lenye kufanana na
ya kule Misri.
Na pia kulikutwa Mawe makubwa yalichongwa yenye kufanana na Wafalme
wa Misri. Na pia kwenye kipindi hiki Wamisri walifanikiwa kufika Palestina na Syria.
Hivyo kipindi hiki kilikuwa ni kipindi cha Wamisri kusambaa.
Na pia kwenye
kipindi hiki ndicho kinazungumzia kuanguka kwa ufalme wa Misri. Kuanguka kwa
ufalme wa Misri ndio ukawa mwanzo wa kuanzishwa utawala wa Warumi mara baada ya
Vita vya Paniki kuanzia miaka ya 300-100 K.K
Aidha kila kipindi kilikuwa na
wafalme wake na malkia wake. Misri ni taifa lililopo upande wa Kaskazini
Mashariki wa Pembe ya Afrikakatika Penisula ya Sinai ambako mpaka wake
unaelekea upande wa bara la Asia.
Misri inapakana na ukanda wa Gaza na Israel
kwa upande wa Kaskazini Mashariki; Ghuba ya Aqaba na bahari ya Shamu kwa upande
wa Mashariki, Sudan kwa upande wa Kusini, Libya kwa upande wa Magharibi na
Bahari ya Mediterrania kwa upande wa Kaskazini.
Lina idadi ya takribani milioni
99 ya watu hiyo ni kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2019.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson…………………………Novemba 11, 2019.
0 Comments:
Post a Comment