Tunisia iliwahi kutawaliwa
na Wafoeniki walioanzisha huko mji wa Karthage.
Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la "Afrika"
katika Dola la Roma.
Kisha eneo lake likaja kutawaliwa na Wavandali, Waarabu,
Wahispaniola, Waturuki na Wafaransa. Ilipata uhuru wake Machi 20, 1956.
Taifa
hilo ni miongoni mwa mataifa yanayopatikana katika ukanda wa Maghreb katika
Afrika ya Kaskazini likipakana na Algeria kwa upande wa Magharibi na Kusini
Magharibi, Libya kwa upande wa Kusini Mashariki na Bahari ya Mediterania kwa
upande wa Kaskazini na Mashariki.
Mnamo mwaka 2017 inakaridiwa kuwa na idadi ya
watu milioni 11.4. Mjini mkuu wa taifa hilo Tunis ulichukuliwa kutokana katika
jina la mama Tunisia, Tunis ipo katika pwani ya Kaskazini Mashariki.
Tunisia
ipo katika pointi ya kaskazini kabisa ya bara la Afrika maarufu Cape Angela.
Ina ukubwa wa Kilometa za Mraba 163,610. Kijiografia taifa hilo kwa upande wa
Mashariki limeundwa na safu za milima ya Atlas na upande wa kaskazini ikiwa ni
Jangwa la Sahara.
Eneo jingine linalosalia katika taifa hilo ni ardhi yenye
rutuba. Baada ya kupata uhuru taifa hili lilijitangazia kuwa Jamhuri ya Tunisia
mnamo mwaka 1957 likiwa mikononi mwa Habib Bourguiba.
Mnamo mwaka 2011
kulitokea mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Rais Zine Abidine ben Ali hivyo
kufanya uchaguzi.
Oktoba 26, 2014 kulifanyika uchaguzi wa bunge la taifa hilo
na uchaguzi wa Rais ulifanyika Novemba 23, 2014. Taifa hilo ni pekee katika
Afrika Kaskazini lenye utawala huru.
0 Comments:
Post a Comment