Novemba 13, 1953 alizaliwa
mwanasiasa wa Mexico ambaye kwa sasa ni Rais wa taifa hilo Andrés Manuel López
Obrador. Amekuwa akifahamika kwa kifupi
kama AMLO.
Aliingia madarakani kwa sanduku la kura mnamo mwaka 2018 hivyo
kuweka rekodi ya kuwa Rais wa 58 wa taifa hilo. Alizaliwa katika mji wa
Tepetitan uliopo katika manisapaa y macuspana Kusini Mashariki mwa jimbo la
Tabasco. Lopez Obrador alihitimu masomo ya chuo kikuu katika chuo kikuu cha
taifa cha Mexico mnamo mwaka 1986 kwenye masomo ya siasa. Alipata shahada yake
ya kwanza katika masuala ya Sayansi ya Siasa. Alianza harakati za kisiasa mnamo
mwaka 1976 akiwa mwanachama wa chama wa PRI katika jimbo la Tabasco. Aliwahi
kuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Indigenous ya Tabasco mnamo mwaka 1977. Akiwa katika
nafasi hiyo Lopez Obrador aliboresha uandishi wa vitabu kuhusu taasisi hiyo.
Mnamo mwaka 1989 alijiunga na Chama cha PRD na mnamo mwaka 1994 aliwania kuwa
Gavana wa Tabasco. Alikuwa kiongozi wa PRD kitaifa kati ya mwaka 1996 hadi
1999. Mnamo mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Serikali mjini Mexico City.
Mnamo mwaka 2012 aliachana na chama cha PRD na kuanzisha chama chake mnamo
mwaka 2014 kinaitwa MORENA ambacho alikuwa mwenyekiti hadi mwaka 2017. Lopez
Obrador amekuwa akichukuliwa kuwa mtu wa watu na anayependwa pia mzalendo.
Amekuwa mashuhuri nchini Mexico kwa zaidi ya miongo miwili. Mnamo mwaka 2018
aliingia katika uchaguzi uliompa kushika madaraka makubwa ya taifa hilo baada
ya kupita katika duru tatu akipambana na mgombea wa mrengo wa kushoto wa chama
cha Labour Juntos Haremos Historia. Morena ni chama cha mrengo wa kulia katika
siasa zake. Katika uchaguzi huo Lopez Obrador alipata asilimia 53 ya kura
katika uchaguzi huo.
0 Comments:
Post a Comment