Wednesday, November 27, 2019

Homa ya Lassa yamuondoa duniani Dr. Noulet Woucher

Daktari kutoka Uholanzi aliyeambukizwa virusi vya homa ya Lassa na kulazwa katika Hospitali ya Masanga, Tonkolili nchini Sierra Leone amefariki dunia. 

Dkt. Noulet Woucher ni miongoni mwa madaktari kumi kutoka barani Ulaya, saba miongoni mwao wakiwa Waholanzi na watatu ni Waingereza. 

Madaktari hao waliondolewa wikiendi iliyopita  kutokana na kuibuka kwa virusi vya homa hiyo inayosababishwa na virusi vya Lassa.

Kwa mujibu wa Afisa Afya wa Wilaya hiyo Dkt. Abdul Mac Falama amesema Mholanzi huyo alipatwa na virusi hivyo na baadhi ya raia wa Sierra baada ya kufanya upasuaji kwa mwanamke mmoja mjamzito aliyekuwa akitokwa na damu nyingi ambaye alifariki dunia baadaye. 

Kutokwa na damu ni miongoni mwa dalili za kuwa na homa ya Lassa pia kuwa na homa kali. 
Hadi sasa kumekuwa juhudi za kupambana na virusi hao wa Lassa kutokana na kwamba mamia ya wagonjwa wamekuwa wakimiminika mahospitalini kwa ajili ya kupata afya. 

Wilaya mbili za Kenema na Kailahun zilizopo Mashariki mwa Sierra Leone zimebainika kuathirika zaidi na virusi vya Lassa. Matukio 300 hadi 400 kwa mwaka yamekuwa yakiripotiwa. 

Homa ya Lassa pia imeenea katika nchi za Liberia na Nigeria.

CHANZO: SIERRA LEONE

0 Comments:

Post a Comment