Zaidi ya watu laki mbili wengi
wao wakiwa watoto wameyakimbia makazi yao baada ya mafuriko kuishika Somalia ya
Kati kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Watu wamekuwa wakiokolewa tangu jana
Alhamisi Okotoba 31 kutokana na janga hilo. Vyombo kama matrekta, boti zimekuwa
zikitumika kwa ajili ya kuwaokoa walioathiriwa na mvua hizo katika mkoa wa
Beledweyne.
Maelfu ya watu wamehamishiwa katika makambi ya muda huku uhitaji
mkubwa ukiwa ni vyakula na maji. Shirika la kutoa misaada ya kiutu la Save the
Children limesema wafanyaka wake wanaendelea kufanya kazi bila kuchoka lakini
kumekuwa na upungufu wa vitendea kazi ili kukabilia na tatizo hilo.
Mkurugenzi
wa shirika hilo Mohamud Mohamed Hassan amesema misaada ya kiutu inatakiwa ili
kuwasaidia walioathirika na kwamba hali inaweza kuwa ngumu na hatari ya kutokea
kwa magonjwa kama malaria na kipindupindu.
CHANZO: CNN
0 Comments:
Post a Comment