Novemba 9, 1877 alizaliwa
mshairi, falsafa, mwanataaluma na mwanasiasa wa nchini Pakistan Muhammad Iqbal.
Iqball anachukuliwa kuwa ndiye muhamasishaji mkuu wa vuguvugu la Pakistan miaka
ile ya 1940 katika eneo zima la British India kama ilivyokuwa ikifahamika. Licha
ya kufariki dunia kwa kiongozi Aprili 21, 1938, mwanasiasa huyo nchini Pakistan
humwita Baba wa Kiroho wa Pakistan. Iqbal anachukuliwa kuwa nembo kuu katika
Fasihi ya Urdu ambapo Iqbal alifanya kazi katika jamii ya Urdu na Uajemi. Kwa
wapenda ushairi Iqbal amekuwa akifuatiliwa na Wahindi, Wapakistan, Wabangladesh,
Wairan na wanataaluma wengine ulimwenguni. Ana majina mengi lakini
linalofahamika sana ni Allam Iqbal. Licha ya kwamba amekuwa akifahamika kama
mshairi mashuhuri lakini bado amekuwa akichukuliwa na Waumini wa Kiislamu kama
Mwanafalsafa wa Kiislamu katika zama za kisasa. Kitabu chake cha kwanza cha
ushairi cha The Secrets of the Self ambacho alikiandika kwa lugha ya Kiajemi
mwaka 1915, pia kazi nyingine za ushairi kwa lugha ya Kiurdu zipo nyingi lakini
mashuhuri ni kama The Call of the Marching Bell, Gabriel’s Wing, The Rod of
Moses na Gift from Hijaz. Mnamo mwaka 1922 alitunukiwa heshima ya mwaka mpya ya
Knight Bachelor na Mfalme George V wakati akisoma sheria na falsafa nchini
England. Iqbal alikuwa mwanachama wa All India Muslim League katika tawi la
London. Jumatatu ya Desemba 29, 1930 alitoa hotuba ambayo inaelezwa kuwa
mashuhuri ya Allahabad Address katika mkutano wa kilele wa 25 wa All-India Muslim
League. Hotuba hiyo inaelezwa kuhamasisha kuanzishwa kwa Dola la Kiislamu
Kaskazini Magharibi mwa India. Serikali ya Pakistan ilishamtangaza Allama Iqbal
kuwa Mshairi wa Taifa hilo na kwa kumheshimu iliamua kutenga siku yake ya
kuzaliwa kama siku ya mapumziko “Yōm-e Welādat-e Muḥammad Iqbāl.” Nyumba
aliyokuwa akiishi Iqball maeneo ya Sialkot bado ipo eneo hilo na inatunzwa kwa ajili ya wageni
wanaitembelea kujua historia mbalimbali za mshairi huyo. Nyumba hiyo
inafahamika kama Iqbal’s Manzil. Lakini pia nyumba nyingine ambayo aliishi
maisha yake yote hadi kifo chake ipo mjini Lahore, ambayo inafahamika kwa jina
la Javed Manzil. Makumbusho yake yapo katika barabara ya Allama Iqbal karibu na
Stesheni ya Treni ya Laore, Punjab nchini Pakistan. Makumbusho hiyo inalindwa
kwa sheria ya Punjab Antiquities ya mwaka 1975 na ilitangaza kuwa makumbusho ya
taifa la Pakistan mnamo mwaka 1977.
0 Comments:
Post a Comment