Eritrea ni taifa ambalo
lipo katika Pembe ya Afrika ambalo mji mkuu wake ni Asmara.
Limepakana na Sudan kwa
upande wa Magharibi na Ethiopia kwa upande wa Kusini. Pia limepakana na na
Djibouti kwa upande wa Kusini Mashariki. Upande wa Kaskazini Mashariki na
Mashariki wa taifa hilo ni pwani ya Bahari ya Shamu.
Taifa hilo lina ukubwa wa
kilometa za mraba 117,600 ikiunganishwa na Dahlak Archipelago na Visiwa vya
Hanish.
Eritrea ni jina la Kigiriki kwa asili ambalo inaelezwa kuwa lilianza
kutumika na Italia waliokuwa wakiishi Italia mwaka ya 1890. Eritrea ni jina
ambalo Wagiriki waliipa Bahari ya Shamu. Hivyo ni jina jingine la Bahari ya
Shamu. Taifa hilo linaundwa na makabila mbalimbali huku makabila tisa
yakitambulika sana na kuchukua idadi kubwa ya watu.
Lina takribani watu milioni
5 hivyo kuliweka kuwa taifa la 116 duniani kwa idadi ya watu. Watu wa taifa
hilo huzungumza zaidi lugha za Kisemitiki ambacho kimechanganyikana na Kiafrika
na lugha baadhi za Asia (Afroasiatic).
Jamii za Watingrinya wanachukua
takribani asilimia 55 ya watu wa taifa hilo. Pia wapo Watigre wanaochukua
asilimia 30 ya watu katika ardhi hiyo. Pia katika lugha kwa nyongeza wapo pia
wanaouzungumza KiNilotiki katika baadhi ya makabili kwenye taifa hilo.
Idadi
kubwa ya watu wa taifa hilo ni Waislamu na Wakristo. Katika historia ya kale
unaposoma Dola la Axum katika karne ya kwanza na ya pili baada ya Kristo basi
ujue kuwa lilikuwa katika ardhi ya Eritrea wakati huo ilikuwa ni kaskazini ya
Ethiopia.
Kuundwa kwa Eritrea ya sasa ni matokeo ya uhuru wa baadhi ya falme
kama zile za Medri Bahri na Ausa ambazo ziliunda kile kilichofahamika kama
Italian Eritrea. Baada ya kushindwa kwa Waitaliano katika vita mwaka 1942.
Hivyo basi Mwingereza akaishika Eritrea mnamo mwaka 1952. Umoja wa Mataifa
ulifikia maamuzi kuwa Eritrea iwe huru.
Eritrea ni nchi ya chama kimoja ambayo
uchaguzi haujawahi kufanyika tangu ilipotangaziwa uhuru wake. Kwa mujibu wa
ripoti za Human Rights Watch zinaeleza kuwa serikali ya Eritrea ni miongoni mwa
serikali ulimwenguni ambazo kiwango cha Haki za Binadamu kipo chini mno.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson............................Novemba 5, 2019
0 Comments:
Post a Comment