Novemba
29, 1932 alizaliwa Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac.
Alizaliwa kwa
mwana wa meneja wa kampuni moja ya ndege Abel Francois Marie Chirac (1898-1968) na mama Marie-Louise
Valette (1902-1973) ambaye alikuwa mama yake.
Mababu zake Jacques walikuwa wakulima lakini mabibi zake wawili walikuwa walimu kutoka Sainte-Fereole.
Chirac alikuwa mwamini wa kanisa Katoliki. Alipoingia madarakani kuiongoza Ufaransa alifanya mabadiliko makubwa ya kisiasa ikiwamo kupunguza muhula wa rais kutoka miaka saba hadi mitano.
Alionekana kama mpinzani mkuu wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq 2003. Alihudumu kama kiongozi wa taifa kutoka 1995 hadi 2007 huku afya yake ikidorora tangu wakati huo.
Pia alihudumu kama waziri mkuu wa Ufaransa, lakini akakabiliwa na msururu wa kesi za ufisadi. Mwaka 2011 alihukumiwa kwa kuchukua fedha za umma alipokuwa akihudumu kama Meya.
Aliugua kiharusi 2005 na mwaka 2014, mkewe Bernadette alisema kwamba hatazungumza hadharani akidai kwamba alikuwa na matatizo ya kiakili kulingana na chombo cha habari cha Ufaransa.
Alikuwa rais wa Ufaransa aliyehudumu kwa muda mrefu baada ya kumrithi Francois Mitterrand. Alipiga vita mpango wa kutokuwpo kwa muungano wa Ulaya na kupigania katiba ya Ulaya ambayo ilikataliwa na wapiga kura ya Ufaransa.
Alifariki dunia asubuhi ya Septemba 26, 2019 akiwa na familia yake kutokana na maradhi ya kiharusi. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

0 Comments:
Post a Comment