Tuesday, November 26, 2019

Liberia ni taifa la namna gani?


Liberia na Sierra Leone ni nchi mbili pekee duniani zilizoanzishwa na kudhibitiwa na Ukoloni hivyo kuendelea kuakisi dhana ya uhuru wa bendera. 

Madhumuni makuu kwa nchi hizi ilikua ni ziwe dampo la watu weusi wanaoachwa kwa sababu mbalimbali huko ughaibuni na hasa watumwa na watu wasio na tija (wachovu, wafungwa sugu, watukutu na fukara wa kupindukia) na hili hasa lilitokea baada ya Mapinduzi ya viwanda ambapo mashine zilianza kutumika kama mbadala wa kazi zilizofanywa na watu/watumwa.  

Liberia Kimsingi Haijawahi kuwa chini ya Ubedui ingawa kimsingi imekua Bedui tangu kuanzishwa kwake kwani ilianzishwa na Chama cha Kikoloni cha Marekani na hapo ndipo eneo lililotengwa kwa ajili ya watumwa walioachiwa huru na ndio maana ya neno Liberia yaani The Land of The Free na hata Mji mkuu wa nchi hiyo Monrovia unaakisi jina la Rais wa Marekani Monroe James kadhalika Katiba na Muundo wa Serikali. 

Bendera ya Liberia inashabihiana sana na Ile ya Marekani ingawa na ile michirizi kumi na moja inatajwa kama ni kiwakilishi cha watu 11 waliosaini mkataba wa uhuru (bendera) lakini kuna mengi nyuma ya pazia hasa kwa hiyo nyota moja. 

Ni miongoni mwa nchi chache Afrika ambapo karibu makabila yote yanapatikana na hii ni kutokana na ukweli kwamba nchi hiyo ilikua kama dampo la watumwa walioachiwa huru na kasi iliongezeka baada ya Mapinduzi ya Viwanda. 

Historia ya Liberia inashabihiana kidogo na Sierra Leone (Lion Mountains) yenye mji pia unaoitwa Free Town, ingawa Sierra Leone (The Province of Freedom) yenyewe ilikua dampo la waingereza masikini ( London's "Black Poor" Province) na ndio maana nchi hiyo ina machotara wengi. 

Licha ya Kuongozwa na Rais mwanamke wa kwanza kabisa Afrika (Iron Lady),na mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel Ellen Johnson Sirleaf; Pia mwaka 2006; Liberia iliweka rekodi ya mwanamke wa kwanza kuingia jeshini nchini humo. 

Taifa hilo limepakana na Sierra Leone kwa upande wa Kaskazini Magharibi, Ivory Coast kwa upande wa Mashariki na Bahari ya Atlantiki kwa upande wa Kusini-Kusini Magharibi. Liberia inachukua kilometa za mraba 111,369. 

Ina idadi ya watu milioni 4,900,000. Lugha ya taifa hilo ni Kiiingereza lakini ndani yake kuna zaidi ya lugha za makabila 20 zinazungumzwa kwenye taifa hilo.

Imetayarishwa na Jabir Johnson......................Novemba 26, 2019


0 Comments:

Post a Comment