Novemba
28, 1820 alizaliwa mwanafalsafa, mkomunisti, mwanasayansi, mwandishi wa habari
na mfanyabiashara wa Ujerumani Friedrich Engels.
Baba yake alikuwa mmiliki wa
kiwanda kikubwa cha nguo mjini Salford nchini England na Barmen huko Prussia
ambayo kwa sasa ni Wuppertal nchini Ujerumani. Engels anafahamika sana kutokana
na kusimamia miongozo ya Karl Marx na kanuni zake. Mnamo mwaka 1845 alichapisha
kitabu kuhusu hali za wafanyakazi nchini England alichokiita “The Condition of
Working Class in England” akiwa amejikita katika utafiti alioufanya na
kuushuhudia kwa macho yake. Engels alizaliwa Barmen, katika jimbo la Rhine,
Prussia akiwa ni mtoto wa Friedrich Engels Sr. (1796-1860) na mama Elisabeth ‘Elise’
Franziska Mauritia von Haar (1797-1873). Alizaliwa katika familia yenye uwezo
ambayo ilikuwa ikimiliki kiwanda cha pamba
huko Barmen na Salford. Wazazi wa Engels walikuwa waamini waaminifu wa Kiprotesanti.
Akiwa na miaka 13 Engels alianza shule ya Gymnasium iliyokuwapo mjini Elberfeld
lakini alipofikisha miaka 17 alilazimishwa kuachana na shule hiyo ya kujifunza
lugha kwani baba yake alitaka mwanaye huyo kuwa mfanyabiashara ili aweze
kufanya kazi katika viwanda vyake. Baada ya muda kitambo kupita Engels hiyo
ilikuwa mwaka 1838 alipelekwa mjini Bremen ili kuishi katika nyumba ya
kibiashara ikiwa ni mkakati wa kuanza kumzoesha masuala ya biashara. Mnamo
mwaka 1842 akiwa na miaka 22 alipelekwa jijini Manchester, England. Kwa wakati
huo ukuaji wa viwanda. Alianza kufanya kazi katika ofisi za Ermen and Engels ambako
ilikuwa ni kiwanda cha kutengeneza kamba. Mnamo mwaka 1848 wakiwa na Marx
waliandika The Communist Manifesto. Hawakuishia hapo katika uandishi huo
walishirikiana kuandika kazi nyingine. Engels alikuwa akimwezesha sana Marx
kifedha ambazo zilimsaidia kufanya utafiti mbalimbali na kuandika Das Kapital. Baada
ya kufariki dunia kwa Marx Engels alihariri kazi za Marx hususani Das Kapital.
Mnamo mwaka 1884 alichapisha kitabu “The Origin Of the Family, Private Property
and the State. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na maradhi ya
kansa Agosti 5, 1895 na majivu yake yalimwagwa huko Beachy Head karibu na
Eastbourne; Mashariki mwa Sussex nchini England.
0 Comments:
Post a Comment