Waziri wa Ushafirishaji wa
Morocco Abdelkader Amara amefunguka kuhusu hali halisi ya wananchi wa taifa
hilo wanaoishi katika maeneo yasiyofikiwa kiurahisi kuwa inapofika wakati wa baridi
hupatwa na matatizo makubwa.
Amara amesema mikoa 27 ya Morocco joto lake hupungua
kipindi cha mwezi Desemba. Takribani raia 736,000 wa taifa hilo hujikuta katika
wakati mgumu wakati anguko la theluji linapofika katika maeneo hayo.
Hata hivyo
wanaharakati nchini humo wanasema serikali inapaswa kuchukua hatua ili
kuwasaidia watu hao katika maeneo hayo yasiyofikiwa kirahisi.
Waziri huyo wa
Usafirishaji amesema wanajipanga kukabilia na changamoto hiyo ikiwamo kupeleka
madaktari 2,480 ambao watatoa msaada wa kitabibu.
Pia Amara amesema kutakuwa na
vituo 745 vya kutoa huduma na magari ya dharura 465 kwa ajili ya wagonjwa.
Hatua hiyo inaonekana kutiliwa shaka na Rais wa Chama cha Mabalozi wa Mazingira
na Mshikamano Ikbal Hafidi ambaye anasema haamini kama hatua hizo zilizotajwa
na waziri wa usafirishaji zitafanyika kwa usahihi.
Wakati huo huo Vyombo vya
Ulinzi na Usalama nchini humo vimekamata kilo 476 za dawa za kulevya aina ya
Cocaine karibu na mji mkuu Rabat.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema madawa
hayo ya kulevya yalikamatwa katika kitongoji cha Harhoura siku ya Jumanne
Novemba 19 mwaka huu. Aidha maofisa polisi wamesema walivamia nyumba moja
iliyopo kilometa 22 kutoka Rabat katika mji wa Temara uliopo kati ya Rabat na
Casablanca.
Maofisa wa polisi waliwakamata wanawake wawili wenye umri wa miaka
40 na mwingine miaka 38 katika operesheni hiyo.
CHANZO: Morocco News
0 Comments:
Post a Comment