Libya ni taifa ambalo lipo
katika ukanda wa Maghreb katika Afrika ya Kaskazini ikipakana na bahari ya
Mediterrania kwa upande wa Kaskazini, Misri kwa upande wa mashariki, Sudani kwa
upande wa Kusini Mashariki, Chadi kwa upande wa Kusini, Niger kwa upande wa
Kusini Magharibi.
Pia Liya imepakana na Algeria kwa upande wa Magharibi na Tunisia
kwa upande wa Kaskazini Magharibi. Taifa
hilo limeundwa na mikoa mitatu ya kihistoria ya Tripolitania, Fezzan na
Cyrenaica. Ina ukubwa wa kilometa za miraba milioni 1.8.
Libya ni taifa la nne
kwa ukubwa barani Afrika likishika nafasi ya 16 ulimwenguni. Taifa hilo
limethibitisha kuwa na hazina kubwa ya mafuta likishika nafasi ya 10
ulimwenguni. Mji Mkuu wa taifa hilo ni Tripoli.
Ina takribani watu milioni sita
ambapo kati yao milioni moja wanaishi Tripoli; huku mji wa pili kwa ukubwa ni
Benghazi uliopo Mashariki mwa taifa hilo.
Historia ya Libya inahusu
eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Libya. Wakazi
asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki
upande wa mashariki.
Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo
ukaenea. Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi. Katika
karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao. Mwaka 1551 Waturuki
walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.
Nchi ilitawaliwa
na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941. Waingereza waliacha nchi mwaka 1951
mikononi mwa mfalme mwenyeji.
kupindua mfalme Idris I, Muammar al-Gaddafi
alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011. Baada
ya hapo vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi sasa.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson……………………………………Novemba 12, 2019
0 Comments:
Post a Comment