Monday, November 25, 2019

Ould El Kharchi lawamani baada kukesha kwa mtoto wa Rais Abdel Aziz

Mohamed Yahya Ould El Kharchi

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Mauritania vinasema Mbunge Mohamed Yahya Ould El Kharchi ameshinda kwa kikao usiku mzima katika mji wa Tafragh Zeina uliopo Magharibi mwa Mji mkuu Nouachott. 

Aidha taarifa hizo zinasema katika mkutano huo Kherchi aliongozana na timu ya wabunge  kwa ajili ya kumuunga mkono Rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz. 

Waliohudhuria mkutano huo wametajwa na kuwa ni  Naibu wa jimbo la Benshab Aali Ould el-Dawla pia manaibu 12 wanaunda muungano wa katika chama kinachotawala cha UPR. 

Wakijibu kuhusu uvumi huo wamesema kuwa uungaji mkono wa mtoto huyo wa Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh Ghazouani ni jambo la kiutamaduni tu na wala sio vinginevyo. 

Inaelezwa kuwa Kherchi ni miongoni mwa wnaaopigia chapuo kufanyiwa mabadiliko ya katiba ambayo yatamwezesha Ould Abdel Aziz  kuwania kwa kipindi cha tatu. Ombi hilo lilisainiwa na manaibu akali ya 100 kabla ya kukatizwa na kauli ya Rais ambaye alikuwa akihutubia  kupitia vyombo vya habari. 

Mauritania Today imesema kuwa mkutano huo uliofanyika nyumbani kwa mtoto wa Abdel Aziz na kuwapo kwa Ould Kharchi ni suala la kifamilia kwa watu wa kabila la Kharchi.


CHANZO: RIM Today

0 Comments:

Post a Comment