Mahakama moja mjini Algiers nchini Algeria imewaachia huru
wafungwa watano wa kisiasa waliokuwa wameshikiliwa katika jela ya El Harrach
kutokana na kukutwa wakiwa wamevaa nembo ya Amazigh iliyopigwa marufuku nchini
humo.
Wafungwa hao Boudjemil Mohand, Idir Ali, Karoun Hamza, Lekhel Kamel na
Okbi Akli walishikiliwa tangu Juni 23 mwaka huu. Mahakama hiyo ya Bab El Oued
iliwakuta hawana hatia na kuwaachia huru.
Nje ya mahakama hiyo hadhira ya watu
zikiwamo familia za wafungwa hao, wanachama wa makundi ya utetezi, vyama vya
wanaharakati, waandishi wa habari walionekana mapema asubuhi ya Novemba 14
kusubiri uamuzi wa mahakama hiyo iliyopo magharibi mwa mji mkuu Algiers.
Baada
ya kuingia mahakama hapo Hakimu wa mahakama hiyo alitaka utulivu wakati akisoma
shitaka hilo. Baada ya kumaliza na kutangaza uamuzi wa kuwaachia wafungwa hao
vilio na kelele za furaha zilidhihirika kwa hadhira hiyo huku wengi wao wakiwa
na simu za viganjani kuchukua tukio hilo.
Umati wa watu walisikika wakitoa
sauti mbele ya Polisi, “ Algeria, Huru na Demokratiki, Sisi ni Imazighen,
Hakuna wa Kutuzuia”. Mbunge aliyejitambulisha kwa jina la Fetta Sadat
alikaririwa na vyombo vya habari kuwa jaji wa mahakama hiyo amesimamia sheria.
“Nina furaha kuona hakika imetendeka lakini ninasikitika
kuona kwa takribani miezi mitano wafungwa hawa wameshikiliwa jela bila sheria
yoyote kuhusika,” alisema Sadat.
Bendera ya Amazigh ikoje?
Nembo hiyo ni ya kiharakati kwa jamii ya watu wa Beriberi
ambayo huwa inatumika na watu mbalimbali wengi wao wakiwa waandamanaji,
wanaharakati wa kisiasa na kitamaduni.
Bendera hiyo ilizinduliwa katika
kitongoji cha Wadya, mjini Kabylia kwenye jimbo la Tizi Wezzu nchini Algeria na
mwanajeshi wa zamani wa Algeria Youcef Medkour.
Miaka ya 1970 Chuo kimoja cha
Waberiberi kianzisha bendera hiyo. Mnamo mwaka 1998 kongamano la dunia la
Amazigh liliidhinisha bendera hiyo maeneo ya Tafira huko Las Palmas de Gran
Canaria katika visiwa vya Canary.
Mnamo Juni 2019 Jenerali Ahmed Gaid Salah alisema
bendera hiyo haiwezi kuvumilika katika maandamano nchini humo Algeria.
Bendera
hiyo ina rangi za Panamazigh ikiwa na mistari mitatu ya ulalo yenye urefu na
upana sawa ikiwa na rangi ya bluu, kijani na njano; aidha katikati ya bendera
hiyo na rangi nyekundu katika herufi Yaz ambayo ni alfabethi ya 30 katika lugha
ya Kiberiberi.
Kwa sasa bendera hiyo imechukuliwa na wanaharakati katika nchi
10 za barani Afrika Morocco, Algeria, Tunisia, Libya, Mauritania, Mali, Niger,
Burkina Faso, Misri na Visiwa vya Canary.
CHANZO: EL WATAN
0 Comments:
Post a Comment