Licha ya katazo la Umoja wa
Mataifa UN la vifaa vya kivita katika ardhi ya Libya lakini juhudi hizo
hazijafanikiwa kuzuia matumizi ya silaha zisizo na rubani.
Matumizi ya ndege zisizo na
rubani katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya zimeufanya mgogoro
huo kuchukua sura nyingine. Kilometa 10 nje kidogo ya mji mkuu wa Libya Tripoli,
Ain Zara kumeshuhudia idadi kubwa ya wanajeshi wanaendelea kujipanga kwa ajili
ya mapigano katika mji mkuu huo.
Tangu Khalifa Haftar aanzishe vita Aprili 4
mwaka huu kwa ajili ya kuushikilia mji huo kila upande umekuwa ukipata msaada
wa hali na mali kutoka kwa marafiki zao nje ya Libya hivyo kulifanya taifa hilo
uwanja wa vita.
Katika mji wa Magharibi wa Misrata majeshi ya Haftar yamekutana
na sauti kutoka angani. Baada ya uchunguzi zaidi wa ndege hizo zisizo na rubani
zimedaiwa ni za Falme za Kiarabu au Saudi Arabia. Gazeti la New York Times
limedai kuwa zaidi ya matukio 900 ya ndege zisizo na rubani yametokea katika
kipindi cha miezi sita iliyopita kwa pande mbili zinazopinga.
0 Comments:
Post a Comment