Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, November 30, 2019

Jela miezi mitatu (3) kwa kutelekeza familia



Mahakama ya Mwanzo ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro imemhukumu mkulima na mkazi wa Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi kwenda jela miezi mitatu na baada ya kumaliza kifungo kutoa shilingi 50,000 kila mwezi baada ya kupatikana na hatia ya kutelekeza familia yake kwa miaka saba.

Hayo yamejiri baada ya mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Akwilina Boniface Mwase (38), Mama Lishe na Mkazi wa Bonite kuithibitishia mahakama pasipo shaka yoyote namna mshtakiwa aliyefahamika kwa jina la Exaud Martin Urassa (55), kuitelekeza familia yake tangu mwaka 2012.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Adnan Kingazi alisema mlalamikaji alimshtaki mshtakiwa kwa shtaka moja la kutelekeza familia kwa mujibu wa kifungu cha sheria Na. 166 na 167 ya kanuni ya adhabu.

Awali mahakama baada ya kupokea ushahidi ilijiuliza hoja za msingi kwamba je, viini halisi vinavyounda shtaka la wizi vimetimia? Pia kwamba je, kuna ushahidi kuwa mshtakiwa ametelekeza familia kama alivyoshtakiwa? Na kwamba je, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka la wizi dhidi ya mshtakiwa katika kiwango kinachostahili cha kutokuacha chembe ya shaka?

Hakimu Kingazi alisema katika kujibu hoja hizo mahakama ilijikita zaidi katika ushahidi uliotolewa na pande zote mbili  ili kuthibitisha shtaka lolote la jina kisheria ni lazima pawepo na nia ovu na tendo ovu la mshtakiwa.

Aidha Kingazi alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi wote watatu wa upande wa mashtaka ulionyesha kufanana kwa kiasi kikubwa na waliloliona ni kwamba mstakiwa mwenyewe alikiri kushindwa kutoa matunzo kwa familia yake toka aondoke nyumbani kwa mke wake.

Pia Mshtakiwa aliiambia mahakama namna alivyoondoka na kumuacha mke wake akiwa na mtoto.

Mshtakiwa aliiambia mahakama kuwa matunzo alitoa mara moja tu kiasi cha Tshs. 35,000/= mwezi januari mwaka 2019 na hadi sasa hajawahi kutoa tena kutokana na kukosa kipato.

Ilidaiwa mahakama hapo kuwa kati ya mwezi June 2018 hadi 2019 nyakati tofauti tofauti huko katika maeneo ya Bonite, Manispaa ya Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro mshtakiwa kwa makusudi na bila halali huku akifahamu kuwa ni kosa alimtelekeza mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 mhitimu wa darasa la saba bila kumpatia matunzo na huduma nyingine muhimu kwa mtoto kitendo ambacho ni kosa na kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana shtaka lake aliposomewa ndipo upande wa mashtaka walipotakiwa kuthibitisha shtaka hilo.

Mlalamikaji aliambia mahakama kwa uchungu namna ambavyo mshtakiwa kama mume wake alivyomtelekeza na mtoto toka mwaka 2012 hadi kufikia uamuzi wa kwenda Ustawi wa Jamii ambapo walimuamuru mshtakiwa atoe Tshs. 75,000/= kwa mwezi.

Mshtakiwa aligoma kutoa kiasi hicho na alipobanwa sana alitoa Tshs. 35,000/= shtaka hilo linafikishwa mahakamani hapo alikuwa hajawahi kutoa chochote.
Kifungu cha Sheria Na. 166 na 167 (Sura ya 16 ya kanuni ya adhabu)

Ilidaiwa mahakamani hapo Ofisi ya Ustawi wa Jamii waliwapa barua ili waende Ofisi ya Dawati la Jinsia Polisi ambako walihojiwa na mshtakiwa aliamriwa atoe matunzo akaendela kukataa ambapo Mlalamikaji aliomba apewe kila mwezi Tshs. 50,000/= pamoja na gharama nyingine za shule na matibabu.

Kwa upande mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13, aliiambia mahakama kuwa hajawahi kuona mshtakiwa (yaani baba yake) akitoa matunzo ya kitu chochote na kuongeza hata vifaa vya shule mama yake ndiye aliyekuwa akimnunulia. Pia mtoto huyo alisisitiza kuwa mshtakiwa hakuwahi kumuuliza chochote kuhusu maendeleo yake shuleni.

Ushahidi wa upande wa mlalamikaji uliendelea kutolewa mahakamani hapo ambako Omari Saidi Kubingwa (80), Balozi wa nyumba 10 eneo walilokuwa wakiishi mshtakiwa na mlalamikaji kama mke na mume aliiambia mahakama namna alivyoitwa na mlalamikaji mwaka 2012 na kumshuhudia mshtakiwa alifungasha virago na kuondoka nyumbani.

Alipomuuliza kwanini anatoa vyombo na kuondoka alidai kuwa amechoshwa na tabia za mke wake za kurudi usiku kila siku.

Shahidi huo aliongeza kuwa alimuuliza mlalamikaji kuhusu tabia hiyo alikana na kusema kuwa mume wake ndiye aliyekuwa akiondoka usiku na kurudi asubuhi. Aliendelea kumsihi sana mshtakiwa asiondoke bila mafanikio.

Katika utetezi wake mshtakiwa alikana kabisa kuitelekeza familia. Mshtakiwa aliiambia mahakama kuwa walianza kuishi na mlalamikaji toka mwaka 2005 na 2006 walimzaa mtoto huyo.
Mshtakiwa aliongeza kuwa waliendelea kuishi pamoja hadi mwaka 2008 ambapo mlalamikaji alianza kwenda Semina za maombi na kurudi usiku sana.

Alidai mahakama hapo kuna wakati alikuwa akimuuliza na mlalamikaji alimwambia nabii amekuwa akiwaamuru kuishi hivyo. Mshtakiwa aliiambia mahakama kuwa mnamo mwaka 2012 maumivu yalimshinda na aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba za wageni yaani gesti ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kupangisha maeneo ya Uswahilini.

Hata hivyo katika shtaka hilo ilidaiwa mahakama hapo mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 mhitimu wa darasa la saba aliwahi kufanyiwa vitendo vya ukatili wakati alipokuwa akiishi kwa baba yake huyo ambaye alioa mke mwingine.

Mtoto huyo alifukuzwa na mlalamikaji kwa madai kuwa baba yake ameondoka nyumbani na amfuate huko aliko ambapo mtoto huyo alikwenda kwa mshtakiwa na mshtakiwa alimpokea mtoto.
Mwaka 2017 mtoto huyo alibakwa na alitoa taarifa polisi. Mtoto alifikishwa hospitali na baada ya kupimwa alionekana kubakwa, kuumizwa na kusababishiwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Mtuhumiwa wa ubakaji alikamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi ambako mwaka jana 2018 alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela.

Hakimu Kingazi alisema mshtakiwa alishindwa kumlinda mtoto Princes wakati akiishi naye hadi kusababisha kubakwa na kusababishiwa maumivu makali mwilini mwake.

Kibaya zaidi ni kwamba badala ya kumfariji mtoto huyo mke mdogo wa mshtakiwa aliendelea kumfanyia mtoto vitendo vya kikatili ikiwamo kumchapa vibaya hadi kumsababishia majeraha mwilini mwake hadi walimu walimshangaa mtoto.

Kitendo hicho kilisababisha walimu kutoa taarifa Ofisi ya Dawati la Jinsia Polisi ambapo waliwaita wazazi wote wa mshtakiwa na kuwahoji kuhusu tukio hilo.

Ilielezwa mahakama hapo kuwa mbakaji mbakaji tayari ameshahukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani mwaka jana (2018) baada ya kupatikana na hatia na kwamba kilichobaki ni ukatili aliotendewa na mama ndogo wake.

Hakimu Kingazi alitoa maelekezo kuwa uchunguzi ufanyike upya na ikibainika mama mdogo huyo alimfanyia mtoto kitendo cha ukatili basi apelekwe mahakamani kujibu shtaka na hatimaye sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha Hakimu Kingazi alisema mshtakiwa amepunguziwa adhabu yake kutokana na sababu za maombolezo alizozitoa kuwa anategemewa na familia nyingine ambapo anaye mtoto mchanga na wazazi wake wote ni wazee na wanamtegemea yeye.

STORY BY: Jabir Johnson..........................Novemba 30, 2019.

MAKTABA YA JAIZMELA: Winston Churchill ni nani?


Novemba 30, 1874 alizaliwa mwanasiasa, mwanajeshi na mwandishi wa vitabu wa Uingereza Winston Churchill. 

Alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1940 na 1945 ambaye alitoa mchango mkubwa wa taifa lake kushinda katika Vita vya Pili vya Dunia. 

Pia alikuja kushika wadhifa huo tena kwa mara ya pili mnamo mwaka 1951 hadi 1955. 

Katika kipindi chote cha uhai wake, muda wake mwingi aliutumia kwenye uongozi na uandishi, alipata nafasi za uongozi kwenye ngazi mbalimbali kwa miaka 55 (tangu mwaka 1900 mpaka 1955, akiwa mbunge kwa kipindi chote, waziri kwa miaka 31 na waziri mkuu kwa miaka 9) na pia aliweza kuandika vitabu zaidi ya 40.

Friday, November 29, 2019

Childreach Tanzania ilivyopenya kwenye makundi maalum

Meneja wa Childreach Tanzania Bi Winfida Kway akimkabidhu cherehani  Afisa Elimu Maalum wawilaya ya Moshi Ladislaus Tarimo.
Meneja miradi wa Childreach Tanzania Bi. Winfrida Kway, alisema watu wenye ulemavu mara kwa mara katika maisha yao ya  kila siku wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kubaguliwa, kutengwa na kukataliwa kutokana na ulemavu wao hivyo Childreach Tanzania  imeona ni vema wahitimu hao ikawapatia vitendea kazi hivyo ambavyo vitaweza kuwasaidia kwenda kuanzisha viwanda vidogo vidogo.


Aidha alisema Childreach Tanzania pia imeweza kujenga miradi mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa darasa kwa ajili ya kusomea na kufanyia mafunzo ya vitendo, uboreshaji wa vyoo ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na miundombinu mizuri ya kiafya ili kuweza kunguza magonjwa ya mlipuko.

“Mwaka 2017 hadi mwaka 2019 shirika la childreach Tanzania kupitia mradi wake wa mafunzo kwa vitendo limeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi 23 kwa kuwawezesha vifaa mbalimbali kama vile vyerehani, vitambaa vya kushonea nguo na vifaa vya useremala, ikiwa ni pamoja na  mahitaji mengine yote muhimu,”alisema.










Wanne wafariki kwa homa ya Ini wilayani Hai, Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Helga Mchomvu akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo Novemba 28,2019.

Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imesema , inaendelea na mapambano dhidi ya uwepo wa ugonjwa wa homa ya ini, baada ya watu wanne kugundulika kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Hai Freddy Kaduma, aliyasema hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani wakati akijibu swali la Diwani wa kata ya Machame Uroki Robson Kimaro,  katika swali lake Kimaro alitaka kujua ni mikakati gani ambayo seriakali ya wilaya hiyo, imeichukua ili kuhakikisha inadhibiti ugonjwa wa homa ya ini ambao umekuwa tishio katika wilaya hiyo.

Kaduma alisema ugonjwa wa huo kwa sasa hivi umeanza kuwa tishio katika wilaya Hai, na kwamba halmashauri ya wilaya ya hiyo, tayari imekwishaanza kuchukua mikakati  ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa  kuwaelimisha jamii jinsi  ya kukabiliana nao.

“Ni kweli ugonjwa huu upo katika wilaya yetu ya Hai, tayari kuwa watu kadhaa wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambao  unaenezwa kwa njia ya ngono isiyo salama, kugusana, kujamiana  na ugonjwa huu unafafana kabisa na ugonjwa wa UKIMWI, endapo mgonjwa atabainika kuambukizwa na ugonjwa wa homa ya ini chanjo hiyo haitafanya kazi,”alisema.

Alisema serikali ya wilaya imeanza kuweka nguvu  kubwa kwa ajili ya kutoa elimu  katika jamii ili kuwaelimisha wananchi kutokana na ugonjwa huo ambao unaenea kwa kasi ili waweze  kwenda kupata chanjo mapema.
“Tayari  jambo hili tumeshaliwasisha katika ngazi ya Mkoa  ili waweze kutuletea dawa za chanjo, ili tuweze kuwachanja wananchi wote, lakini chanjo hizi zitakuwa zalipiwa na sio bure,’alisema.

Katika swali lake la msingi diwani Robson Kimaro, alisema ndani ya kata yake watu wanne wametajwa kufariki kutokana na ugonjwa huo, halmashauri imeweka nguvu gani ili kuhakikisha ugonjwa huo hauendelei kuenezwa katika maeneo mengine.

“Homa ya ini ni ugonjwa ambao umeanza kuenea kwa kasi kubwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Hai, na katika kata yangu watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa huo, serikali imechukua hatua gani katika kukabiliana na tatizo hilo?,”alihoji Kimaro.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Masama Kusini Elingaya Massawe, aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kwamba idara ya afya inakwenda kufanya mikutano kwa wananchi ili kuwapata elimu ya kutosha jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo.

STORY & PHOTO BY: Kija Elias, Moshi
DATE: Novemba 28, 2019







MAKTABA YA JAIZMELA: Jacques Chirac ni nani?


Novemba 29, 1932 alizaliwa Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac. 

Alizaliwa kwa mwana wa meneja wa kampuni moja ya ndege Abel Francois  Marie Chirac (1898-1968) na mama Marie-Louise Valette (1902-1973) ambaye alikuwa mama yake. 

Mababu zake Jacques walikuwa wakulima lakini mabibi zake wawili walikuwa walimu kutoka Sainte-Fereole. 

Chirac alikuwa mwamini wa kanisa Katoliki. Alipoingia madarakani kuiongoza Ufaransa alifanya mabadiliko makubwa ya kisiasa ikiwamo kupunguza muhula wa rais kutoka miaka saba hadi mitano. 

Alionekana kama mpinzani mkuu wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq 2003. Alihudumu kama kiongozi wa taifa kutoka 1995 hadi 2007 huku afya yake ikidorora tangu wakati huo. 

Pia alihudumu kama waziri mkuu wa Ufaransa, lakini akakabiliwa na msururu wa kesi za ufisadi. Mwaka 2011 alihukumiwa kwa kuchukua fedha za umma alipokuwa akihudumu kama Meya. 

Aliugua kiharusi 2005 na mwaka 2014, mkewe Bernadette alisema kwamba hatazungumza hadharani akidai kwamba alikuwa na matatizo ya kiakili kulingana na chombo cha habari cha Ufaransa. 

Alikuwa rais wa Ufaransa aliyehudumu kwa muda mrefu baada ya kumrithi Francois Mitterrand. Alipiga vita mpango wa kutokuwpo kwa muungano wa Ulaya na kupigania katiba ya Ulaya ambayo ilikataliwa na wapiga kura ya Ufaransa. 

Alifariki dunia asubuhi ya Septemba 26, 2019 akiwa na familia yake kutokana na maradhi ya kiharusi. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Thursday, November 28, 2019

Chuo Cha Maendeleo ya Jamii FDC Same chapokea Sh Milioni 647

Jengo la chuo cha maendeleo ya jamii, likiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Serikali  imetoa fedha zaidi ya Sh milioni 600 kwa ajili ya kukarabati Chuo Cha Maendeleo ya Jamii, huku ikiwaonya watu watakaobainika kuzitumia vibaya fedha hizo serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule, wakati alipokuwa akikabidhi fedha hizo kwa mkuu wa chuo cha FDC  ambapo alisema kuwa mtu yeyote atakayebainika kuzitumia fedha hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa  atazitapika fedha hizo.

DC Senyamule alisema fedha za serikali zinapokuja zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kwamba  serikali haitasita kumchukulia hatua  kali za kisheria.

“Serikali Kuu imetoa Sh  milioni 647 kwa chuo cha FDC Same, ili ziweze kutumika kwa ajili ya kukarabati majengo yote, kujenga bweni, madarasa mawili, jengo la utawala, karakana ya magari pamoja na darasa la wanafunzi wa shule ya awali.”alisema.

Aidha  DC Senyamule, alimtaka mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii FDC Same, kuhakikisha anasimamia kikamilifu shughuli za ujenzi huo huku akimtaka mkandarasi huyo kumaliza kazi kwa  muda uliowekwa na serikali.

"Rais Dkt. John Magufuli anayafanya haya yote ili  wanafunzi ambazo hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya juu  waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri ama kuajiriwa kutokana na fani ambazo mmezipata kutoka katika chuo hiki.”alisema.

Alisema mradi wa kukuza ujuzi na stadi za ajira ulianzishwa kwa lengo la kutekeleza vipaumbele vya serikali vilivyoainishwa katika mkakati wa serikali wa kufikia Tanzania ya Viwanda ifikapo 2025, lakini pia kuwezesha vijana kupata ujuzi kwa vitendo kuliko nadharia pamoja na kujengea uwezo vyuo vya kati.

“Namshukuru sana Rais Dkt. Magufuli kwa kuweza kutupatia wilaya ya Same fedha kwa ajili ya kukarabati chuo hiki, kwani chuo hiki kilikuwa kimesahaulika kwa miaka mingi mno na miundombinu ya majengo haya yalikuwa machakavu, lakini kutokana na fedha hizi sasa matumaini mazingira ya chuo yataboreka," DC Same.
Itakumbukwa kwamba serikali ilianzisha vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (VMW) kwa madhumuni ya kuimarisha maarifa na stadi kwa wananchi ili waondokane na ujinga, umaskini na maradhi na hatimaye kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

“Vyuo hivi vilianzishwa kwa lengo la kumtayarisha mtanzania ambaye ni mtu mzima aweze kukuza utu wake na kumfanya awe kamili katika jumuiya ya Watu wake, aweze kutumia akili zake vizuri na kuweza kuamua mambo  yake au ya umma kwa njia iliyo sahihi, ikiwa ni pamoja na kufikia kiwango cha juu zaidi katika ufundi wa kazi anazozifanya,”alifafanua.

Naye  Mwenyekiti wa Bodi John Mwasi, ameitaka jamii kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto viziwi  huku pia akitoa rai kwa wale wenye uwezo kutoa fursa za ajira  kwa vijana hao.

Nao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho katika risala yao iliyosomwa kwa niaba yao  na Salim Elia, walisema wanakabiliwa na uhaba wa walimu wa ufundi, vifaa vya ufundi  hasa useremala zikiwemo mbao za kufanyia mazoezi ya vitendo na vitambaa kwa ushonaji.

“Tunaishukuru serikali kwa kutuletea umeme chuoni hapa, lakini changamoto iliyopo ni kwamba  tangu umeme huo uletwe haujaweza kusambazwa kwenye mabweni na kwenye karakana ya kujifunzia hali ambayo inakuwa ngumu kwetu kujifunza kutokana na changamoto hiyo ya umeme,”alisema.

Mwajuma Hemedi, ameomba kuwepo kwa fursa za mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana tunaohitimu mafunzo ya ufundi stadi kwani wanahitaji kujiajiri wenyewe kama walivyofanya baadhi ya wenzao. 


Childreach Tanzania yawasaidia viziwi msaada wa Cherehani, vifaa vya useremala


 
Wahitimu wa Chuo cha ufundi Ghona kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameaswa kuanzisha viwanda vidogo vidogo  ili ziwasaidie katika kuanzisha miradi yao ya kiuchumi .

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Childreach Tanzania Martha Lyimo,  wakati  alipokuwa akikabidhi jana vyerehani na vifaa vya useremala kwa wahitimu hao ambao ni viziwi katika mahafali yao nane chuoni hapo.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Meneja miradi wa Childreach Tanzania Bi. Winfrida Kway, alisema watu wenye ulemavu mara kwa mara katika maisha yao ya  kila siku wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kubaguliwa, kutengwa na kukataliwa kutokana na ulemavu wao hivyo Childreach Tanzania  imeona ni vema wahitimu hao ikawapatia vitendea kazi hivyo ambavyo vitaweza kuwasaidia kwenda kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Bi. Winfridah Kway
Bi. Winfrida Kway, alisema shirika limeweza kutekeleza miradi  mbalimbali ndani ya chuo cha Ghona kwa kushirikiana na serikali pamoja na wana jamii ikiwa ni  sehemu ya kuwawezesha  kufikia malengo endelevu ya milenia ya mwaka 2030 pamoja na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa watu wenye ulemavu ya mwaka 2003.

“Mwaka 2017 hadi mwaka 2019 shirika la childreach Tanzania kupitia mradi wake wa mafunzo kwa vitendo limeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi 23 kwa kuwawezesha vifaa mbalimbali kama vile vyerehani, vitambaa vya kushonea nguo na vifaa vya useremala, ikiwa ni pamoja na  mahitaji mengine yote muhimu,”alisema.

Aliongeza kusema kuwa “Wanafunzi wa fani ya useremala  hupewa nyenzo zote muhimu za kuweza kujiajiri pindi wanapo rudi majumbani huku  wanafunzi wa fani za ushonaji nao pia huwezeshwa vifaa kama vile vyerehani na vitambaa,”alisema.

Aidha alisema Childreach Tanzania pia imeweza kujenga miradi mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa darasa kwa ajili ya kusomea na kufanyia mafunzo ya vitendo, uboreshaji wa vyoo ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na miundombinu mizuri ya kiafya ili kuweza kunguza magonjwa ya mlipuko.



Miradi mingine ni  uchimbaji wa kisima cha maji,  ili kuwawezesha upatikanaji wa maji shuleni  kwa matumizi mbalimbali, mradi wa duka, mradi wa mbuzi, mradi wa ng’ombe wa maziwa na mradi wa ufugaji wa kuku.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo Afisa Elimu Ufundi Halmashauri ya Moshi  Ladislaus Tilya, alisema endapo wahitimu hao wataitumia vyema taaluma waliyoipata wataweza kujitengenezea ajira na hata kuajiri watu wengine.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya chuo, Mkuu wa Chuo hicho Aminiel Mwanga  alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 2010 na umoja wa wazazi wenye watoto walemavu Kanda ya Kaskazini (UWAVIKA), wanafunzi hao wamefaidika na mafunzo mbalimbali, ambayo yamekuwa yakitolewa chuoni hapo.
“Lengo la kuanzishwa kwa kituo hiki ni kuwasaidia watoto viziwi ambao wanamaliza elimu ya msingi na hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari na waliohitimu elimu ya sekondari  na hawakupata mahali pa kujifunza stadi mbalimbali za kiufundi zitakazowasaidia kujitegemea  wao wenyewe,”alisema.

"Mbele yako kuna vijana 10 viziwi  wakiwemo wasichana 5 na wavulana 5 ambao wamehitimu leo mafunzo yao ya ufundi yaliyodumu kwa muda wa miaka mitatu, wahitimu hao walijifunza masomo ya taaluma kama vile Hisabati , kiingereza , Kiswahili, uraia, ujasiriamali na stadi za maisha pia wamejifunza masomo ya ushonaji kwa wasichana na wavulana walijifunza useremala, uchomeleaji kama masomo ya misingi ya ufundi,"alisema Mwalimu Mwanga.

STORY BY: Kija Elias, Moshi
DATE: Novemba 27, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Friedrich Engels ni nani?


Novemba 28, 1820 alizaliwa mwanafalsafa, mkomunisti, mwanasayansi, mwandishi wa habari na mfanyabiashara wa Ujerumani Friedrich Engels. 

Baba yake alikuwa mmiliki wa kiwanda kikubwa cha nguo mjini Salford nchini England na Barmen huko Prussia ambayo kwa sasa ni Wuppertal nchini Ujerumani. Engels anafahamika sana kutokana na kusimamia miongozo ya Karl Marx na kanuni zake. Mnamo mwaka 1845 alichapisha kitabu kuhusu hali za wafanyakazi nchini England alichokiita “The Condition of Working Class in England” akiwa amejikita katika utafiti alioufanya na kuushuhudia kwa macho yake. Engels alizaliwa Barmen, katika jimbo la Rhine, Prussia akiwa ni mtoto wa Friedrich Engels Sr. (1796-1860) na mama Elisabeth ‘Elise’ Franziska Mauritia von Haar (1797-1873). Alizaliwa katika familia yenye uwezo ambayo ilikuwa ikimiliki kiwanda cha pamba  huko Barmen na Salford. Wazazi wa Engels walikuwa waamini waaminifu wa Kiprotesanti. Akiwa na miaka 13 Engels alianza shule ya Gymnasium iliyokuwapo mjini Elberfeld lakini alipofikisha miaka 17 alilazimishwa kuachana na shule hiyo ya kujifunza lugha kwani baba yake alitaka mwanaye huyo kuwa mfanyabiashara ili aweze kufanya kazi katika viwanda vyake. Baada ya muda kitambo kupita Engels hiyo ilikuwa mwaka 1838 alipelekwa mjini Bremen ili kuishi katika nyumba ya kibiashara ikiwa ni mkakati wa kuanza kumzoesha masuala ya biashara. Mnamo mwaka 1842 akiwa na miaka 22 alipelekwa jijini Manchester, England. Kwa wakati huo ukuaji wa viwanda. Alianza kufanya kazi katika ofisi za Ermen and Engels ambako ilikuwa ni kiwanda cha kutengeneza kamba. Mnamo mwaka 1848 wakiwa na Marx waliandika The Communist Manifesto. Hawakuishia hapo katika uandishi huo walishirikiana kuandika kazi nyingine. Engels alikuwa akimwezesha sana Marx kifedha ambazo zilimsaidia kufanya utafiti mbalimbali na kuandika Das Kapital. Baada ya kufariki dunia kwa Marx Engels alihariri kazi za Marx hususani Das Kapital. Mnamo mwaka 1884 alichapisha kitabu “The Origin Of the Family, Private Property and the State. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na maradhi ya kansa Agosti 5, 1895 na majivu yake yalimwagwa huko Beachy Head karibu na Eastbourne; Mashariki mwa Sussex nchini England.

Wednesday, November 27, 2019

Homa ya Lassa yamuondoa duniani Dr. Noulet Woucher

Daktari kutoka Uholanzi aliyeambukizwa virusi vya homa ya Lassa na kulazwa katika Hospitali ya Masanga, Tonkolili nchini Sierra Leone amefariki dunia. 

Dkt. Noulet Woucher ni miongoni mwa madaktari kumi kutoka barani Ulaya, saba miongoni mwao wakiwa Waholanzi na watatu ni Waingereza. 

Madaktari hao waliondolewa wikiendi iliyopita  kutokana na kuibuka kwa virusi vya homa hiyo inayosababishwa na virusi vya Lassa.

Kwa mujibu wa Afisa Afya wa Wilaya hiyo Dkt. Abdul Mac Falama amesema Mholanzi huyo alipatwa na virusi hivyo na baadhi ya raia wa Sierra baada ya kufanya upasuaji kwa mwanamke mmoja mjamzito aliyekuwa akitokwa na damu nyingi ambaye alifariki dunia baadaye. 

Kutokwa na damu ni miongoni mwa dalili za kuwa na homa ya Lassa pia kuwa na homa kali. 
Hadi sasa kumekuwa juhudi za kupambana na virusi hao wa Lassa kutokana na kwamba mamia ya wagonjwa wamekuwa wakimiminika mahospitalini kwa ajili ya kupata afya. 

Wilaya mbili za Kenema na Kailahun zilizopo Mashariki mwa Sierra Leone zimebainika kuathirika zaidi na virusi vya Lassa. Matukio 300 hadi 400 kwa mwaka yamekuwa yakiripotiwa. 

Homa ya Lassa pia imeenea katika nchi za Liberia na Nigeria.

CHANZO: SIERRA LEONE

Sierra Leone ni taifa la namna gani?

Sierra leone ni nchi inayopatikana magharibi mwa bara la Afrika, mji mkuu wake unaitwa Freetown ambao ndiyo mji mkubwa ukifuatiwa na mji wa Bo. Nchi hii inapakana na Guinea kwa upande wa kaskazini, upande wa kusini-mashariki inapakana na Liberia na kusini magharibi bahari ya Antlantiki. Sierra leone inaukubwa wa kilometa za mraba 71,740.

Nchi hii imegawanyika katika sehemu nne yaani, mkoa wa kaskazini, magharibi, kusini na mashariki.
Kuna makabila 16 na kila moja likiwa na lugha yake na utamaduni wake. 

Lakini makabila yaliyo makubwa ni Wamende na Watemne.nchi hii ni ya kiislamu kwa asilimia 60, huku asilimia 30 ikichukuliwa na dini za kiafrika na asilimia 10 ikichukuliwa na ukristo.

Asili ya neno Sierra Leone lilitokea mnamo mwaka 1462 wakati mreno aliyejulikana kwa jina la Pedro da Cintra alipofika eneo hilo na kukuta mlima ukiwa umesimama (leo hii ni Penisula ya Freetown) , ndipo alisema kwa Kireno Serra da Leoa ikiwa na maana ya Milima ya Simba  na baadaye kutamkwa Sierra Leone.

Historia inasema Sierra Leone ilipata uhuru kwenye miaka ya 1961, ambapo harakati za uhuru ziliongozwa na Milton Margai (waziri mkuu wa kwanza) kutoka katika utawala wa Uingereza. Ukweli ni kwamba Siera Leone ni moja ya nchi iliyobarikiwa kuwa na utajiri wa madini ya almasi.

Wananchi walidhani maisha yatabadilika kutokana na utajiri huo, lakini baada ya uhuru serikali haikufanya mabadiliko, kwani wananchi waliendelea kuwa maskini na asilimia kubwa ya rasilimali zilkuwa zikifaidiwa na wachache wenye madaraka, na wazungu kutoka ulaya. 

Hata Wananchi waliokuwa wakichimba madini hayo walikuwa na hali mbaya, huku wakiwanufaisha wafanyabiashara kutoka nje.

Ndipo hali ilibadilika kwenye miaka ya 1980 palipoundwa kundi lililojulikana kama RUF (Revolutionary United Front) lilikuwa likipinga serikali ya Joseph Momo. 

Mpaka kufikia miaka 1991 machafuko yalianza na takribani watu wengi walipoteza maisha huku wengine wakiachwa na vilema na bila kusahau wengine wakiwa wakimbizi. 

RUF waliamini kuwa Serikali iliyopo madarakani ilichaguliwa na wananchi, kumbe ubovu wa serikali unasababishwa na Wanachi. 

Hivyo kwa kuwa mtu anapiga kura kwa kutumia mikono, basi RUF walikuwa wakiwakata watu mikono huku wakisema “NO MORE HAND, NO MORE VOTE”.

mpaka mwaka 2002 machafuko hayo yaliisha baada ya jeshi la nchi kuingilia kati na umoja wa mataifa pia. Ndipo kukawa na mikataba ya amani.

Mpaka sasa kuna familia ni maskini, kuna familia zimepoteza watu wao, na jambo la kusikitisha machafuko hayo yalihusisha mauaji yaliyokuwa yakifanywa na watoto wadogo waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya. Lengo la RUF lilkuwa kuwakomboa wananchi na walitaka rasilimali zitumike kwa ajili ya wananchi wote.

Kwa sasa Sierra Leone ni moja ya nchi ambayo inakumbwa na janga la ugonjwa wa Ebola.

Imetayarishwa na Jabir Johnson..........................Novemba 27, 2019.

Tuesday, November 26, 2019

DJ Khaled atimiza miaka 44

Novemba 26, 1975 alizaliwa mwanamuziki maarufu wa Marekani ambaye amekuwa akifahamika kwa jina la DJ Khaled. 

Huyu ni prodyuza, DJ, mtunzi wa nyimbo na mtu anayejihusisha sana na vyombo vya habari. Jina lake halisi ni Khaled Mohamed Khaled. 

Alizaliwa New Orleans huko Louisiana. Khaled alianza kufahamika kwa mara ya kwanza wakati akiwa mtangazaji wa kipindi cha redio moja mjini Miami miaka ile ya 1990. 

Alikuwa mtangazaji katika kipindi cha Hip hop katika Redio 99 Jamz huko huko jimboni Florida. Umaarufu wake ulilifanya kundi la Terro Squad lenye maskani yake jijini New York katika viunga vya Bronx kumkodi kwa ajili ya matamasha mubashara ya majukwaani. Baada ya hapo Khaled alipambana na kuanza kutoa albamu ambapo mwaka 2006 aliachia albamu ya Listennn.....the Album ambayo ilijipatia cheti chenye hadhi ya juu. 

Mwaka uliofuata alitoa alabamu ya We the Best ambayo ilikuwa na singo 20 miongoni mwa hizo ni ile ya I’m so Hood. Mwaka 2008 na 2010 aliachia albamu mbili ya We Global na Victory. Hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuwa na lebo yake amabyo aliita We the Best Music Group. 

Albamu hizo mbili zilipanda vizuri katika orodha ya 10 bora za US Billboard 200; ndani hizo albamu kulikuwa na singo nyingine kali ya All I do is Win ambayo nayo ilijipatia cheti cha hadhi ya Platinum. Mnamo mwaka 2011 aliachia albamu yake ya tano  aliyoipa jina la We the Best Forever ambayo ilifanya vizuri sokoni na kumpa umaarufu mkubwa. Kuna wimbo wa I’m on One ulifanya vizuri mno na kuwa katika orodha ya 10 bora. 

Albamu ya sita nay a saba alizotoa mwaka 2012 na 2013 ambazo ni Kiss the Ring na Suffering from Success. Albamu hizo zilipanda hadi kuwa katika 10 bora za Billboard 200. Albamu ya nane aliitoa mwaka 2015 yenye jina la I changed a Lot. 

Mwaka 2015 na 2016 umaarufu wa DJ Khaled ulipanda na kuushawishi ulimwengu kuanza kumfuatilia kwa kina ikiwamo mitandao ya kijamii na vituo mbalimbali vya redio na televisheni. Aliachia albamu ya tisa mwaka 2016 ya Major Key. 

Albamu ya kumi aliiachia mwaka 2017 aliyoipa jina la Grateful. Mwaka huu ameachia albamu ya Father of Asahd ambayo imeshika namba mbili katika Billboard 200. Pia DJ Khaled ameandika kitabu chenye jina la The Keys ambacho kimefanya vizuri katika soko. Na mwaka ujao ataonekana katika filamu ya Bad Boys for Life