Friday, January 31, 2020
In memory of Rasual Butler and Leah LaBelle
Januari 31, 2018 alifariki dunia mchezaji wa kimataifa wa mchezo wa kikapu wa Ligi Kuu nchini Marekani (NBA) Rasual Butler.
Nyota huyo wa kikapu alikuwa mchezaji wa Miami Heat pia aliwahi kuhudumu na New Orleans Hornets, Los Angeles Clippers, Chicago Bulls, Toronto Raptors, Indiana Pacers, Washington Wizards na San Antonio Spurs.
Alicheza kikapu nchini humo kwa miaka 14. Butler alizaliwa Philadelphia Mei 23, 1979. Alisoma na kucheza mpira wa kikapu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha La Salle, Philadelphia. Alipata fura ya kuingia NBA mnamo mwaka 2002 katika drafti ya mzunguko wa pili.
Butler alifariki dunia akiwa na mpenzi wake ambaye alikuwa mwimbaji aliyefahamika kwa jina la Leah LaBelle. LaBelle alizaliwa Toronto, nchini Canada na kukulia jijini Seattle.
LaBelle alianza kuimba tangu akiwa mtoto na alianzia kuimba kwaya katika kanisa. Wakati akihojiwa kwenye kinyang'anyiro cha American Idol alisema anajisikia vizuri kuwa raia wa Marekani na mwimbaji.
Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 31 katika ajali mbaya ya gari. LaBelle alifika fainali za American Idol. Februari 5, 2018 Vyeti vya Vifo vyao vilionyesha kuwa walikuwa bado hawajaowana.
Katika Chumba cha Kuhifadhi Maiti cha Metropolitan jijini Los Angeles mwili wa Butler ulikabidhiwa kwa binti yake mkubwa kwa ajili ya maziko huko Newcastle, Delaware. Mwili mwanadada LaBelle ulitolewa katika chuma cha kuhifadhi maiti cha Forest Lawn huko Los Angeles na kukabidhiwa kwa wazazi wake kwa ajili ya maziko Seattle, Washington.
Wawili hao walipata ajali mbaya ya gari baada ya gari kukosa mwelekeo katika Bonde la San Fernando kwenye kaunti ya Ventura Boulevard huko California.
Inaelezwa wakiwa katika gari aina ya Range Rover ilionyesha kuwa gari lilikuwa katika spidi ya 60mph. Pia taarifa zilisema kuwa miili ya marehemu hao ilikuwa ikiwa na kiasi cha dawa za kulevya hususani mwili wa Butler ulikuwa na kiasi kidogo cha pombe na bangi.
Enzi za uhai wake Butler alikuwa ni mpenzi wa kuendesha vipindi mbalimbali katika televisheni, muziki na kuigiza filamu. Leah LaBelle Vladowski alizaliwa Septemba 8, 1986 .
Alikuwa mwimbaji wa Pop, R&B na Soul. LaBelle aliwahi kufanya kazi na nyota wengine katika muziki Jermaine Dupri, Keri Hilson na Pharrell Williams.
Thursday, January 30, 2020
MAKTABA YA JAIZMELA: Kwanini Mahtma Gandhi aliuawa?
Januari 30, 1948 alifariki dunia mwanasheria, mwanafalsafa, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa siasa nchini India maarufu Mahtma Gandhi.
Gandhi alipigwa risasi na kuuawa akitembea katika bustani ya nyumba huko Delhi. Mwuaji wake alikuwa Mhindu wa kundi lililofuata itikadi kali.
Kijana huyo alikasirishwa na hatua za kupatanisha Waislamu na Wahindu akaamini Gandhi alikuwa msaliti wa Uhindu.Gandhi alijulikana hasa kwa jina la Mahatma. Neno hili la Kisanskrit linamaanisha "roho kubwa".
Aliitwa hivyo mara ya kwanza alipofika Bombay wakati wa kurudi kutoka Afrika Kusini. Gandhi hakupenda jina hilo lakini alishindwa kuzuia matumizi yake. Jina lake halisi ni Mohandas Karamchand Gandhi.
Anajulikana hasa kama kiongozi wa harakati za uhuru wa Uhindi aliyepinga na kushinda ukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi wa mabavu au silaha. Gandhi alizaliwa katika eneo la Gujarat kama mtoto mdogo wa Karamchand Gandhi na mama Putali Bai.
Baba yake alikuwa waziri mkuu katika serikali ya maharaja wa nchi lindwa ndogo ya Porbandar wakati ilipokuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza.
Familia yake ilifuata dini ya Uhindu, madhehebu ya Wavishnu, lakini nyumba ya Gandhi ilitembelewa pia na Waislamu na Wajain. Mwaka 1883 akiwa na umri wa miaka 13 aliozwa kwa mke wake Kasturba wakazaa watoto 4.
Mwaka 1888 alisafiri kwenda Uingereza akasoma sheria kwenye chuo kikuu cha London, akapokewa kama wakili kwenye mahakama za juu kuanzia 1891. Huko Uingereza alisoma mengi juu ya Ukristo, akipendezwa hasa na mahubiri ya Yesu na hotuba ya mlimani, lakini hakuvutwa na nafasi ya pekee Yesu anayopewa katika imani ya Kikristo.
Wakati uleule alianza kusoma vitabu vitakatifu vya Uhindu, hasa Bhagavad Gita iliyoendelea kuwa mwongozo wa kiroho maishani mwake. Baada ya mtihani alirudi Uhindi akafanya kazi kama wakili mjini Bombay.
Mwaka 1893 alitumwa Afrika Kusini kwa kesi moja tu, lakini alibaki huko hadi 1914. Baada ya kuugua aliondoka Afrika Kusini mwaka 1914 akarudi Uhindi alipopokewa kama shujaa kwa sababu habari zake zilimtangulia. Aliunda makazi ya pamoja (ashram) alimoishi na watu waliofuata imani yake ya satyagraha.
Alianza kuvaa nguo za wakulima wa kawaida. Ndani ya Uhindi yenyewe fitina ilianza juu ya nafasi ya Waislamu katika taifa jipya, huku sehemu kubwa ya Waislamu wakidai kugawiwa kwa koloni katika nchi mbili. Mapigano yalianza na watu elfu kadhaa waliuawa.
Mnamo Agosti 1947 nchi mbili za India na Pakistan zilianzishwa, na Oktoba 1947 vita vikafuata kati ya nchi hizo mbili juu ya jimbo la Kashmir. Vita vikaongeza uadui, na watu milioni kadhaa walifukuzwa yaani Wahindu kutoka Pakistan na Waislamu kutoka India.
Gandhi alizaliwa Oktoba 2, 1869
Wednesday, January 29, 2020
Mateo Anthony aifumua Tanzania Prisons
Mshambuliaji wa Polisi Tanzania Mateo Anthony katika dimba la Ushirika, Moshi. |
Polisi Tanzania imeibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara uliochezwa katika dimba la Ushirika Mjini Moshi, Kilimanjaro.
Bao la dakika ya 82 ya
mchezo lilifungwa na Mateo Anthony akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango
Jeremia Kilubi ndani ya eneo la hatari baada ya kazi nzuri ya Erick Msagati na
Sixtus Sabilo waliowapoteza walinzi wa Tanzania Prisons Nurdin Chona na Jumanne
Elifadhil.
Huu ni mchezo wa nane Polisi
Tanzania inashinda tangu kuanza kwa msimu wa 2019/2020 ikiwa imecheza mechi 17.
MAKTABA YA JAIZMELA: Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ni nani?
Januari 29, 1950 alifariki dunia mtawala wa kumi wa taifa la Kuwait Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 65.
Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ni mtoto wa Jaber II Al-Sabah ambaye alikuwa mtawala wa Kuwait kati ya mwaka 1915 hadi 1917.
Aliingia madarakani baada ya kifo cha mjomba wake Salem Al-Sabah ambaye alikuwa mtawala wa tisa wa Kuwait mnamo mwaka 1921 hadi kifo chake.
Baba yake alikuwa kiongozi wa kijeshi na mwanzilishi wa Jeshi la Kuwait pia Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Miaka ya 1920 aligawa madaraka hayo ya kijeshi kwa Ali Salem Al-Mubarak Al-Sabah na baadaye alichukua Sheikh Abdullah Jaber Al-Abdullah II Al-Sabah kutokana na vita ya Regeai.
Vita hii ilitokea Januari 1928 ambayo inachukuliwa kuwa ndiyo vita ya mwisho katika historia ya awali ya Kuwait.
Pia vita hii ilikuwa ya kwanza katika historia ya Kuwait kutumia magari ya kivita. Ilipiganwa zaidi kaskazini Magharibi mwa mji wa Al Jahra nchini humo wakati wa utawala wa Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.
Watu kati ya 200 na 300 waliuawa katika mapigano hayo ambayo yalishuhudiwa Kamanda wa Vikosi vya kijeshi Sheikh Ali Salem Al-Mubarak Al-Sabah akipoteza maisha.
Wakati wa uhai wake Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah alioa mara kadhaa na kuzaa watoto saba miongoni mwao ni Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ambaye ni crown prince wa Kuwait nafasi aliyoichukua mnamo mwaka 2006 hadi sasa.
Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah alifariki dunia katika jumba la Kifalme la Dasman nchini humo.
Alizaliwa mnamo mwaka 1885.
Tuesday, January 28, 2020
Nike yaomboleza kifo cha Kobe Bryant
Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imekuwa miongoni mwa makampuni yalioomboleza kifo cha nyota wa kikapu Kobe Bryant aliyefariki Januari 27, 2020 kwa ajali ya helikopta.
Ilichokifanya kampuni hiyo ni katika bidhaa zote zilizokuwa na zikitumiwa na Kobe Bryant na kuandika maneno yanayoashiria maombolezo.
Nike katika salamu zao za rambirambi ilisomeka
"Tukiwa sambamba na mamilioni ya wanamichezo na mashabiki duniani kote, tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hizi leo. Tunatoa rambirambi zetu kwa familia na marafiki na wote waliokuwa karibu na Kobe na Gianna.
Kobe alikuwa miongoni mwa wanamichezo wakubwa katika kizazi chake na alikuwa na ushawishi mkubwa usioweza kupimika katika ulimwengu wa michezo na jamii nzima ya mpira wa kikapu. Alikuwa mwanachama aliyependwa na familia ya Nike. Tutamkosa sana. Mamba Forever."
MAKTABA YA JAIZMELA: Meja Jenerali Suraj Abdurrhman ni nani?
Januari 28, 2015 alifariki dunia mwanajeshi na mhandisi wa majengo wa Jeshi la Nigeria aliyeongoza mapambano katika ardhi ya Liberia Meja-Jenerali Suraj Alao Abdurrahman.
Mwanajeshi huyo alifariki dunia jijini New York kwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi.
Alisoma shule ya msingi LEA huko Maiduguri Road katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria mnamo mwaka 1961 hadi 1967.
Suraj alifanikiwa kwenda katika vyuo vya serikali kikiwamo cha KEFFI WASC mnamo mwaka 1972. Aliingia katika jeshi la Nigeria mnamo mwaka 1973 na kufanikiwa kuendelea na kozi mbalimbali kuanzia hapo hadi mwaka 1974.
Katika fani ya uhandisi wa majengo alijiunga na chuo cha mnamo mwaka 1976 akaendelea tena katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria kuchukua shahada ya Uhandisi wa Majengo mnamo mwaka 1979.
Mnamo mwaka 1981 alisalia chuoni hapo na kuchukua Shahada ya Uzamili. Shahda yake ya Uzamivu aliichukulia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskochi mnamo mwaka 1985.
Baada ya kuchukua shahada hizo aliendelea kuchukua kozi nyingine za kijeshi ambapo mnamo mwaka 2003 alikwenda katika kozi ya kijeshi ya kimataifa nchini Uingereza Muungano wa Kimataifa.
Wakati anafariki alikuwa na mke mmoja anayetambulika kwa jina la Fatima Wali-Abdurrahman ambaye walizaa naye watoto wanne Surajudeen, Abduljabbar, Abdulaziz na Abdulmalik.
Alikuwa akipendelea zaidi kupiga picha , kusafiri na katika michezo alikuwa mpenzi wa gofu na mpira wa kikapu.
Alizaliwa Septemba 9, 1954.
Mwanajeshi huyo alifariki dunia jijini New York kwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi.
Alisoma shule ya msingi LEA huko Maiduguri Road katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria mnamo mwaka 1961 hadi 1967.
Suraj alifanikiwa kwenda katika vyuo vya serikali kikiwamo cha KEFFI WASC mnamo mwaka 1972. Aliingia katika jeshi la Nigeria mnamo mwaka 1973 na kufanikiwa kuendelea na kozi mbalimbali kuanzia hapo hadi mwaka 1974.
Katika fani ya uhandisi wa majengo alijiunga na chuo cha mnamo mwaka 1976 akaendelea tena katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria kuchukua shahada ya Uhandisi wa Majengo mnamo mwaka 1979.
Mnamo mwaka 1981 alisalia chuoni hapo na kuchukua Shahada ya Uzamili. Shahda yake ya Uzamivu aliichukulia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskochi mnamo mwaka 1985.
Baada ya kuchukua shahada hizo aliendelea kuchukua kozi nyingine za kijeshi ambapo mnamo mwaka 2003 alikwenda katika kozi ya kijeshi ya kimataifa nchini Uingereza Muungano wa Kimataifa.
Wakati anafariki alikuwa na mke mmoja anayetambulika kwa jina la Fatima Wali-Abdurrahman ambaye walizaa naye watoto wanne Surajudeen, Abduljabbar, Abdulaziz na Abdulmalik.
Alikuwa akipendelea zaidi kupiga picha , kusafiri na katika michezo alikuwa mpenzi wa gofu na mpira wa kikapu.
Alizaliwa Septemba 9, 1954.
Monday, January 27, 2020
Kitambi Noma yatoa dozi yaizabua Moshi Veterans Club 3-2
Moshi Veterans Club imeshindwa kutamba katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Kitambi Noma baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-2 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Sekondari ya Ilboru jijini Arusha.
Salehe Salum 'Macheda' alikuwa wa kwanza kuliona lango la Kitambi Noma katika dakika ya 10 baada ya kazi nzuri ya Madesho.
Abdul Madesho ndiye aliyeisawazishia Moshi Veterans Club katika dakika ya 56 ya baada ya kufumua mkwaju uliokufa mita 27 kutoka katika lango la Kitambi Noma na kufanya ubao kusomeka 2-2.
Hata hivyo dakika ya 73 ya mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kutoka na ushindani mkali wa kila upande Sanga Ngomelo alipigilia msumari wa mwisho na kuifanya Kitambi Noma ing'are katika mchezo huo.
Awali Kitambi Nomailifumania nyavu kupitia kwa Muddy Mshana na Kevin Lema katika mchezo huo dhidi ya Moshi Veterans Club.
Mwenyekiti Tumaini Mungete wa MVC alikaririwa akisema, "Asiwepo wa kujitetea, siku zote huwa napenda kusema mchezo una matokeo matatu kushinda, sare na kufungwa, tumekubali wametufunga walikuwa bora kuliko sisi tunawakaribisha Moshi."
Kwa upande wake Msemaji wa Kitambi Noma Ali Msungi alisema mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa nzuri na kwamba wameuanza mwaka vizuri hivyo wanaamini katika mechi zijazo licha ya upinzani kuwa mkali watakuwa na matokeo mazuri.
Salehe Salum 'Macheda' alikuwa wa kwanza kuliona lango la Kitambi Noma katika dakika ya 10 baada ya kazi nzuri ya Madesho.
Abdul Madesho ndiye aliyeisawazishia Moshi Veterans Club katika dakika ya 56 ya baada ya kufumua mkwaju uliokufa mita 27 kutoka katika lango la Kitambi Noma na kufanya ubao kusomeka 2-2.
Hata hivyo dakika ya 73 ya mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kutoka na ushindani mkali wa kila upande Sanga Ngomelo alipigilia msumari wa mwisho na kuifanya Kitambi Noma ing'are katika mchezo huo.
Awali Kitambi Nomailifumania nyavu kupitia kwa Muddy Mshana na Kevin Lema katika mchezo huo dhidi ya Moshi Veterans Club.
Mwenyekiti Tumaini Mungete wa MVC alikaririwa akisema, "Asiwepo wa kujitetea, siku zote huwa napenda kusema mchezo una matokeo matatu kushinda, sare na kufungwa, tumekubali wametufunga walikuwa bora kuliko sisi tunawakaribisha Moshi."
Kwa upande wake Msemaji wa Kitambi Noma Ali Msungi alisema mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa nzuri na kwamba wameuanza mwaka vizuri hivyo wanaamini katika mechi zijazo licha ya upinzani kuwa mkali watakuwa na matokeo mazuri.
Kikosi cha Moshi Veterans Club mwaka 2020 |
Kikosi cha Kitambi Noma mwaka 2020 |
Kocha wa Kitambi Noma akizungumza na wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika |
Mlinzi wa pembeni kulia wa Moshi Veterans Club Hard Core akiondoa hatari langoni mwake dhidi mshambuliaji wa Kitambi Noma. |
Winga wa Kitambi Noma akitafuta njia ya kupita. |
Ilikuwa ni kazi kwelikweli baina ya Kitambi Noma na Moshi Veterans Club katika kufungua mwaka 2020 |
Kobe Bryant na bintiye wafariki dunia katika ajali ya Helkopta
Nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant amefariki dunia kwa ajali ya Helicopter iliyotokea jijini California, nchini humo.
Bryant alikuwa akihudumu na Los Angeles Lakers inayoshiriki ligi kuu ya NBA nchini humo.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 41 na walikuwa watu Tisa akiwemo mwanae Gianna kwenye Helicopter hiyo binafsi na taarifa za awali zinasema chombo hicho kilishika moto ikiwa angani na baadae kudondoka.
Mkongwe wa Kikapu Karim Abdul Jabbar ni miongoni mwa waliomlilia Kobe Bryant.
Kifo cha Suharto (1921-2008)
Januari 27, 2008 alifariki dunia mwanasiasa maarufu wa Indonesia ambaye aliwahi kushika wadhifa wa kuliongoza taifa hilo akiwa Rais wa pili. Huyu anafahamika kwa jina la Suharto. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.
Aliliongoza taifa hilo kutoka Machi 27, 1968 hadi alipojiuzulu Mei 21, 1998. Baada ya kujiuzulu nafasi ya kuliongoza taifa hilo Suharto alikuwa akilazwa mara kwa mara kutoka na kukabiliwa na stroke, maradhi ya moyo na matatizo ya utumbo.
Hata wanasheria wake waliwahi kuwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu kuwa hali yake sio nzuri kwa hiyo hatakuwa na uwezo wa kusimama kizimbani kujibu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Mnamo mwaka 2006 mwanasheria mkuu Abdurrahman alituma timu ya madaktari 20 ili wafanya uchunguzi wa kina kuhusu afya ya Suharto. Daktari mmoja aliyefahamika kwa jina la Brigedia-Jenerali Marjo Subiandono alikaririwa akionyesha wasiwasi wake kwa kusema Suharto ana matatizo mawili katika ubongo wake.
Hata hivyo Januari 4, 2008 Suharto alichukuliwa kwenda katika Hospitali ya Pertamina jijini Jakarta kutokana na hali yake ya afya kuwa dhaifu kwani alikuwa amevimba mikono, miguu na tumbo; pia inaelezwa Suharto alikuwa na matatizo japo sio kwa sana katika figo zake.
Hali ilizidi kuwa dhaifu kwani majuma kadhaa baadaye kulijitokeza anaemia, shinikizo la damu la kushuka kutokana na maradhi ya moyo na figo pia kuvunja kwa damu kwa ndani, mapafu kujaa maji, damu katika haja kubwa na ndogo ambayo ilisababishwa na kushuka kwa kiwango cha haemoglobin.
Januari 23, 2008 hali ya Suharto ilikuwa mbaya zaidi kwani ilijitokeza hali kwa kitaalamu hufahamika kama Sepsisi ambayo mwili huwa unaachia keemikali kwa wingi ili kupambana na maradhi hivyo kemikali hiyo ikisambaa mwili mzima huleta madhara makubwa kwani kila eneo litakuwa halijiwezi.
Familia ya Suharto ilikubaliana na kuwataka madaktari kuondoa vifaa vya usaidizi alivyokuwa amewekewa na ilipofika Januari 27, 2008 saa 7:09 mchana Suharto alifariki dunia.
Dakika chache baada ya taarifa za kifo chake Rais wa Indonesia wakati huo Susilo Bambang Yudhoyono aliita waandishi wa habari na kutangaza kifo hicho huku akimwelezea Suharto kuwa ni miongoni mwa watoto bora wa Indonesia na kuwataka raia wa taifa hilo kutoa heshima kwa rais huyo wa zamani bila kujali madhaifu yaliyojitokeza wakati wa utawala wake.
Mwili wa Suharto ulichukuliwa kutoka Jakarta hadi Giri Bangun jijini Solo katika jiji la Central Java na kuzikwa huko. Suharto alizikwa pembezoni mwa kaburi la mkewe kwa heshima zote za kijeshi.
Rais Yudhoyono na maofisa wa serikali walihudhuria mazishi hayo huku watu wa Indonesia wakisimama katika mitaa na barabarani kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo. Rais Yudhoyono alitangaza juma moja la maombolezo kutokana na kifo cha Suharto.
Alizaliwa Juni 8, 1921 katika kijiji cha Kemusuk kilichokuwa katika dola ya Yogyakarta. Suharto alizaliwa wakati wa utawala wa Wadachi katika Indonesia wakati huo ikiitwa Dutch East Indies.
Alizaliwa katika familia maskini iliyokuwa ikiishi katika nyumba iliyojengwa kwa miti ya mianzi na kusilibwa na udongo katika ardhi ya Wajava. Kiongozi huyo wa kijeshi aliingia madarakani baada ya kumtoa madarakani Sukarno ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo.
Alianza kushikilia hatamu tangu mwaka 1967 hadi alipojiuzulu mwaka 1998. Katika hotuba yake ya kujiuzulu aliowaomba radhi watu wa Indonesia kwa makosa ambayo aliyafanya wakati wa utawala wake.
Suharto alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kemusuk karibu na jiji la Yogyakarta. Alikuwa katika hali ya unyenyekevu. Wazazi wake wa Kijava waliokuwa waumini wa dini ya Kiislamu walitalikiana na kusalia kama wadaawa muda mfupi baada ya Suharto kuzaliwa.
Wakati wa utawala wa Wajapani katika Indonesia, Suharto alihudumu katika Jeshi la Ulinzi la Wajapan. Wakati wa harakati za kupata uhuru kwa taifa hilo alikuwamo katika Majeshi ya Indonesia. Suharto alifanikiwa kupanda cheo na kuwa Meja Jenerali baada ya Uhuru wa Indonesia. Alifanya jaribio la kupindua utawala wa Sukarno (mwasisi wa taifa hilo) na kufanikiwa Septemba 30, 1965 akiungwa mkono na Chama cha Kikomunisti cha Indonesia.
Aliteuliwa kushika nafasi ya urais baada ya jaribio hilo mwaka 1967 na mwaka 1968 alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo.
Aliposhika madaraka hiyo alianza kuongoza taifa hilo kwa kuweka sheria ambazo zilikuwa zikimpa kuitambulika na raia wa taifa hilo.
Suharto alikuwa imara miaka ile ya 1970 hadi 1980. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 hali ilikuwa mbaya katika taifa hilo, ambalo inaelezwa udikteta ulitawala na vitendo vya rushwa. Hali hiyo ilimlazimisha kujiuzulu May 1998.
Wakati wa kujiuzulu kwake aliomba msamaha kwa Waindonesia wote kwa yaliyotokea kwani yalisababisha uchumi wa taifa hilo kubaki nyuma.
Saturday, January 25, 2020
Malameni Rock: Mwamba uliomaliza watoto wa Kipare
Malameni Rock at Mbaga, Same. |
Utamaduni ni jumla
ya mambo yote yaliyobuniwa na jamii ili kukidhi utashi na maendeleo yake.
Kwa maneno mengine
utamaduni ni mwenendo wa maisha ya jamii, mtazamo wao wa mambo na taratibu zao
za kuendesha maisha zinazowatofautisha wao na jamii nyingine.
Utamaduni ndicho
kitambulisho kikuu cha taifa na ni ikielelezo cha utashi na uhai wa watu wake.
Nguzo za Utamaduni ni pamoja na mila na desturi, lugha, michezo na historia.
Kwa mfano katika
baadhi ya mila na desturi za makabila mtoto akizaliwa hakuna mtu anayeruhusiwa
kumwona mtoto huyo.
Kwa kawaida, mtoto huwekwa ndani ya nyumba nao watu wasio
washiriki wa familia hawaruhusiwi kumwona mpaka baada ya sherehe ya kumpa jina.
WILAYA YA SAME,
KILIMANJARO
WILAYA ya Same ipo
Mkoa wa Kilimanjaro umbali wa kilometa 105 kutoka Moshi yalipo Makao Makuu ya
Mkoa.
Ni kati ya Wilaya 6
za Mkoa wa Kilimanjaro. Wilaya ya Same ilianzishwa mwaka 1962.
Kwa mujibu wa
makadirio ya mwaka 2017; Wilaya ya Same inakadiriwa kuwa na Wakazi wapatao
296,287 na idadi ya kaya zipatazo 65,842
Wilaya ya Same ipo
katikati ya Latitudo 040 04’006 Kaskazini hadi 040 04’456 Kusini na Longitudo
370 04’87 Mashariki hadi 380 04’897 Magharibi.
Hali ya hewa ya
wilaya ina kiwango kati ya nyuzi joto 15 hadi 30 na kiwango cha mvua cha
wastani wa kati ya lita za ujazo 500 hadi 2,000 kwa mwaka.
Kiikolojia Wilaya
imegawanyika katika kanda tatu nazo ni; ukanda wa juu ambao ni milimani.
Eneo linalofaa kwa
kilimo cha tangawizi, kahawa, ndizi, maharage, miwa, miti (kwa ajili ya mbao/
boriti/kuni) matunda mbalimbali kama mapapai, na maparachichi.
Ukanda wa kati na ukanda wa chini ambao ni tambarare. Ukanda
wa tambarare katika wilaya ya Same una hali ya kijangwa na makazi mtawanyiko
kwa wakazi wanaojishughulisha na ufugaji.
Hifadhi ya Mkomazi
Hifadhi ya Mkomazi ilianzishwa mwaka 1951 kama Pori la Akiba la Mkomazi –umba,
kutoka katika Pori Tengefu la Ruvu na lina ukubwa wa kilometa za mraba, 3600,
Pori hilo la Akiba lilipandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya Taifa (National
Park).
Hifadhi iko ndani ya
mikoa ya Kilimanjaro katika Wilaya ya Same kwa asilimia 61 na Wilaya ya Lushoto
mkoani Tanga kwa asilimia 39 na ukubwa wa hifadhi nzima ni kilometa za mraba
3245.
HISTORIA YA KABILA
LA WAPARE
Wapare ni kabila
kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania.
Kabla ya kuingia huko, inasemekana walikuwa Taveta, Kenya, kwa zaidi ya karne
moja iliyopita na wakati huo walikuwa wakijulikana kwa jina la Waasu.
Masimulizi yanasema
walipoingia Tanganyika, walitamani kufanya makao yao kwenye miteremko ya Mlima
Kilimanjaro, lakini wakavurumishwa na wenzao waliokuwepo kabla yao, yaani Wachagga.
Wachagga hao
hawakuwa radhi kuwaruhusu Wapare kuwa na makazi eneo hili, hivyo waliwafukuza
kwa kupigana kama ilivyokuwa tabia ya makabila mengi hapo zamani.
Wakati wa kupambana
walikuwa wakiambiana, “Mpare… Mpare” wakimaanisha ‘Mpige…Mpige!’ Waasu hawa
wakatimka mbio na kuparamia milima ambayo sasa inaitwa milima ya Upare. Waasu
wakaanza kuitwa Wapare kwa maana ya "Wapige".
Hizi ni hadithi
zinazosimuliwa na baadhi ya Wachagga ambao ndio watani pekee wa Wapare, utani
uliozaliwa baada ya purukushani hizo za kuingia Tanganyika.
Hata hivyo, hakuna
hata Mpare mmoja anayeafiki maelezo hayo, isipokuwa wanakiri kuwa walitokea
Taveta: ndiyo maana hata baadhi ya maneno na lafudhi yao haiko mbali sana na
watu wa Taveta.
Zamani Wapare
walikuwa na sala tofauti kwa kila ukoo na eneo lao la tambiko.
Katika karne ya 19
hadi 20 wamisionari wa Ukristo waliingia maeneo mengi ya Upare.
Imani za Wapare kwa
sasa zinatofautiana kutokana na maeneo: walio kusini mwa wilaya ya Same katika
maeneo ya Ndungu, Kihurio, Bendera, Hedaru, Makanya, Suji, Chome, Tae, Gonja,
Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisa la Sabato wengi sana.
Maeneo kama Chome,
Mbaga, Gonja, Vudee yana waumini wengi wa Kanisa la Kilutheri.
Katika Wilaya ya
Mwanga kuna idadi kubwa ya Walutheri na Waislamu.
Wakatoliki, japo ni
wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara Juu, Vumari na Mbaga.
MWAMBA WA
MALAMENI ULIVYO
Kimbwereza akitoa maelezo kuhusu Malameni Rock. |
Petrolojia ni tawi
la jiolojia ambalo linasoma miamba na masharti ambayo huyaunda. Petrolojia ina
sehemu ndogo tatu: igneous, metamorphic, na petrology sedimentary.
Hivyo basi muundo wa
Malameni Rock, ni mwamba mgando au mgumu au moto (igneous). Sifa za miamba hii
ambayo kipetrolojia ilitokana na kupoa na kuganda kwa magma.
Hadi mwaka 1930 mila
na desturi za Wapare katika kuwatoa watoto wenye ulemavu wakidai kuwa ni
kuondoa mapepo ambayo yangeweza kuwasababishia laana na mikosi katika familia
hizo zilikuwa zikiendelea kufanya. Hii ikiwa ni kabla ya Wamishionari wa
Kikristo kuanza kueneza neno la Mungu katika milima hiyo ya Upareni.
Miaka ya mwishoni
mwa 1800 ukristo ulianza kupenya katika milima hiyo. Mchungaji mmoja kutoka
Leipzig aliyefahamika kwa jina Jacob Jenson Dannholz alijenga kanisa katika
kijiji cha Mbaga ambako Malameni Rock inapatikana kati ya mwaka 1908 hadi 1917.
Hadi sasa unapofika
katika Vilima vya Mbaga ili uweze kwenda kujionea namna mwamba huo ulivyo, ni
sharti upewe maelekezo na historia kuhusu Malameni Rock.
Kwa kifupi ni kwamba
Malameni Rock haipo mbali na Mapango ya Mghimbi ambayo nayo ya historia yake.
USHUHUDA WA
MCHUNGAJI MARTIN KOSMALLA
Ushuhuda huu ni wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mchungaji Martin Kosmalla ambao aliuhifadhi kwa
njia ya maandishi mnamo mwaka 1932.
"Jana nilikuwa
nikiitwa na mwanamke mara mbilimbili. Niliambiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa na
maumivu makali na kwamba asingeweza kuzaa mtoto," anaanza Mchungaji
Kosmalla katika ushuhuda wake.
"Mtoto wako ni
mzima, anaishi, yu hai hajafa. Ndipo nilipoliona tabasamu nilikionekana kwa
mwanamke yule aliyejawa na huzuni na maumivu makali na alikubaliana na maneno
yangu."
Mchungaji Kosmalla
anasema baada ya tukio lile kupita siku ile, usiku wake akiwa nyumbani kwake
aligongewa na alipotoka nje alikutana na baba wa familia ya yule mwanamke
aliambiwa kwamba mkewe amejifungua mtoto wa kiume na kinachovutia zaidi hali
yake ya afya ilikuwa nzuri na mkewe anaendelea vizuri.
Mwanaume wa kabila
la Wapare anaweza akawa tajiri wa mifugo na mali nyingi lakini pasipokuwa na
watoto basi huonekana kama mtu maskini.
Hali hiyo huwekwa
msisitizo na methali mbalimbali, kwamba mwanaume tajiri bila watoto sifa zake ni bure na utajiri wake
ni nani atakayeulinda.
Mchungaji Kosmalla
anasema licha ya kuzaliwa kwa watoto lakini kwa kabila la Wapare kitu kingine
cha ziada huangaliwa ambacho ni afya ya mtoto huyo.
"Endapo
kutakuwa na hitilafu katika mwili wa mtoto, hofu huikumba familia yote na kifo
itakuwa ndio zawadi pekee mtoto huyo itamfaa," anasema Mchungaji Kosmalla.
Malameni Rock au
Mwamba wa Malameni uliopo katika kijiji cha Mbaga-Manka ndio mahali ambapo
watoto wasio na hatia walikuwa wakiuliwa kwa kuweka juu nyakati za usiku na
mama zao ambao huwanyonyesha na kuwabembeleza hadi usingizi utakapowashika
kisha kuwalaza hapo ili watakapozinduka wataviringika kutoka juu hadi chini na
ndio hadithi yao huishi palepale.
Mama zao baada ya
kuwabembeleza kuondoka hapo kwa machozi makubwa kwani hawatakuja kuwaona tena,
lakini yote hayo ni kwasababu ya ulemavu waliozaliwa nao.
Mchungaji huyo
anasimulia siku moja wakati akiendelea na huduma yake katika milima ya Pare
aliamua kuondoka na waamini wake kwenda katika mwamba ambao ulikuwa ukiangamiza
watoto wengi waliozaliwa wakiwa na ulemavu.
Mchungaji Kosmalla
anasema wakati wa kupanda kwenda katika mwamba huo walikuwa wakipanda taratibu
na kwa uangalifu mkubwa kutokana na mwinuko wake kuwa mkali ili waweze kufika
katika kilele cha mwamba huo na alisimama huko na kuwaambiwa waumini wake.
"Hapa ndio
mahali ambapo watoto wenye ulemavu, wasio na hatia walihukumiwa na mama mwenye
mtoto alikuwa akimbusu mtoto wake kwa mara mwisho na kumwacha hapa asimwone
tena kwani atakapozinduka katika usingizi ataviringika kutoka juu hadi chini na
kupoteza maisha."
DHANA YA ULEMAVU KWA
WATOTO ILIVYOJENGEKA
Muongozaji wa watalii kujionea vivutio Eliakunda akizungumza kuhusu Malameni Rock. |
Kwa mujibu wa kamusi
ya mtandaoni Wikipedia; Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini
au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha ya
jamii.
Unamwekea mtu mipaka
asiweze kutekeleza shughuli fulani katika maisha yake, tofauti na watu wengine.
Kuna nchi nyingi
walemavu wana klabu za michezo au kuendesha michezo katika vitengo vya pekee
vya klabu za kawaida.
Kwa kawaida
wanatekeleza michezo ya kawaida lakini kufuatana na kanuni zinazolingana na
hitilafu zao.
Je, Malameni Rock
iliwahi kufikiria kuwa kuna siku nchi mbalimbali zitakuja kuwa na maendeleo ya
juu ambayo yangemthamini mtoto mwenye ulemavu badala ya kuwaza kuwa anailetea
jamii husika laana na mikosi?
Hivyo basi Malameni
Rock inasalia kuwa ni mwamba wa kihistoria ambao unafaa kuenziwa ili kuendelea
kutoa msisitizo kwa jamii mbalimbali Tanzania na ulimwenguni kote umuhimu wa
kutowatenga watoto wenye ulemavu na wakati mwingine kuwaua kwa kudhani ni mikosi
na laana.
STORY & PHOTO BY: Kija
EDITED BY: Jabir Johnson
MAKTABA YA JAIZMELA: Mamadou Dia ni nani?
Januari 25, 2009 alifariki
dunia Waziri Mkuu wa kwanza wa taifa la Senegal aliyefahamika kwa jina la
Mamadou Dia.
Mwanasiasa huyo wa Senegal alihudumu katika nafasi hiyo kutoka
mwaka 1957 hadi mwaka 1962. Alishika wadhifa huo hadi alipolazimishwa kujiuzulu
na pia mashtaka yake ya kutaka kuipindua serikali ya Rais wa wakati huo Leopold
Sedar Senghor. Dia alianza harakati zake za kisiasa mnamo mwaka 1949 kama
kiongozi wa baraza kuu wa AOF na katibu mkuu wa chama cha Senegalese Democratic
Bloc (BDS) mnamo mwaka 1950. Alihudumu katika bunge la seneti la Ufaransa
kutoka mwaka 1948 hadi mwaka 1956 na pia kama naibu spika wa bunge la Ufaransa
kutoka mwaka 1956 hadi mwaka 1958. Akiwa na Senghor, walifanikiwa kuanzisha
chama cha African Convention (PCA) Januari mwaka 1957 kutoka BDS. Baada ya rais
wa zamani wa Ufaransa Charles de Gaulle kuanzisha utaratibu mwingine wa kisiasa
katika jamii nzima ya Ufaransa na makoloni yake mnamo mwaka 1958 wawili hayo
yaani Senghor na Dia walikuwa wapinzani katika sera zao. Dia alikuwa
akipendelea kujiondoa katika muungano na Ufaransa wakati Senghor alipendelea
kusalia mikononi mwa wakoloni hao. Dia alifanya kazi ya ziada katika mikataba
mbalimbali kwenye taifa hilo dhidi ya wakoloni kutoka barani Ulaya, ambao
walikuwa na nia ya kuinyonya zaidi Senegal. Baada ya miaka miwili ya kuwamo
katika bunge, Mamadou Dia alikuwa mhimili mkuu wa ukosefu wa utulivu baada ya
uhuru wa mwaka 1962 pale ambapo alishindwa kutekeleza jaribio lake la kuipindua
katibu ili amzidi kete mtu wake wa karibu Senghor hapo ndipo maisha yake ya
kisiasa yalipoingia doa na kujikuta akizuiliwa katika jela kwa kitendo hicho.
Licha ya maisha yake ya kisiasa kwa maana ya nguvu kuporwa lakini maisha yake
ya ndani hayakuharibika kwani mnamo miaka ya 1980 alitaka kurudi tena katika
ulingo wa kisiasa baada ya mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa na Abdou Diouf.
Hata hivyo chama kidogo cha The People Democratic Movement hakikupata uungwaji
mkono wa kutosha. Baada ya hapo hakurudi tena katika medani ya siasa ya taifa hilo
na alisalia kuwa nembo ya siasa za Senegal. Hadi leo Mamadou Dia anakumbukwa
kwa mchango wake wa kuitengeneza Senegal ya sasa. Pia anakumbukwa kwa kuwa
mpinzani wa Rais wa sasa wa Senegal Abdoulaye Wade ambaye aliwahi kuwa wakili
wake miaka ile ya 1963.
Mamadou alizaliwa Julai 18,
1910 katika mji wa Khombole, mkoani
Thies na kufariki dunia akiwa na umri wa
miaka 98 jijini Dakar. Siku aliyofariki magazeti yaliandika mengi ya kumsifia
kiongozi huyo kwamba alikuwa mtu aliyefuata kanuni na utaratibu ili kuijenga
Senegal.
UN yataka usaidizi kukabiliana na nzige Afrika Mashariki
Umoja wa Mataifa
umetoa wito wa usaidizi wa kimataifa kukabiliana na nzige wengi waliovamia
maeneo ya Afrika mashariki.
Msemaji wa Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa
msaada ili kukabiliana na athari za nzige kama vile ukosefu wa chakula,
utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.
Ethiopia, Kenya na
Somalia zinapitia wakati mumu kukabiliana na na makundi ya nzige ambako
hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo, limesema shirika la
FAO.
Shirika hilo
linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo
Juni mwaka huu.
Kwa siku moja tu,
kundi la nzige Paris huenda likala kiwango cha chakula kinachoweza kuliwa na
nusu idadi ya watu wote Ufaransa.
Nzige wanaweza
kusafiri umbali wa kilomita 150 (maili 93) kwa siku na kila nzige mkubwa
anaweza kula chakula kiasi kikubwa tu cha chakula kwa siku.
Tatizo hilo
linaendelea kuwa kubwa zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Mbali na nzige hao
kuongezeka maeneo ya Afrika Mashariki, pia wamejitokza katika nchi za India,
Iran na Pakistan, ambao huenda wakabadilika na kuanza kusambaa kwa makundi
ifikapo msimu wa chipukizi
Friday, January 24, 2020
Gazeti la Tanzania Daima Januari 24, 2020: Kangi Lugola
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania John Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo
Kangi Lugola, akisema wizara hiyo inaongoza katika kuchukua miradi ya ovyo.
Rais Magufuli pia amemfuta
kazi Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini humo, Thobias Andengenye
kwa kusimamia mradi usieleweke wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 452.
Rais Magufuli alitangaza
kuwafuta kazi viongozi hao wawili muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa nyumba
za maofisa magereza katika mji wa kibiashara wa Dar es Salaam.
Amesema naibu waziri wa
Mambo ya Ndani Hamad Masauni na katibu mkuu wa wizara hiyo Jacob Kingu
wamemwandikia barua ya kujiuzulu nyadhifa zao na amezipokea.
George Simbachawene aliyekuwa
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira amechukua nafasi ya Kangi Lugola.
Simbachawene anakuwa waziri wa 26 kuchukua nafasi hiyo tangu mwaka 1961. Pia wizara
ya Mambo ya ndani ndiyo wizara ngumu nchini.
Wanafunzi 24 waliotekwa Cameroon waokolewa
Jeshi la Cameroon
limewaokoa wanafunzi 24 waliokuwa wakishikiliwa na waasi wenye silaha katika
eneo linalozungumza Kiingereza la Meme nchini humo.
Ofisa mwandamizi wa eneo
hilo Ntou Ndong Chamberlain amesema, watoto hao walitekwa nyara mapema Jumanne
kwenye shule yao iliyopo kusini magharibi mwa mji wa Kumba na kupelekwa katika
msitu ambako kuna kambi ya waasi. Waasi wawili waliuawa kwa risasi katika
operesheni ya uokoaji, na silaha na risasi zimekamatwa.
Watoto hao wenye umri wa
miaka mitano hadi 10 wamerudishwa kwenye familia zao.
CHANZO: CRI Swahili