Thursday, October 31, 2019
Ufahamu mwezi Novemba
Novemba ni mwezi wa pili wa
mwisho katika kalenda ya Gregori. Mwezi huu upo katikati ya mwezi Oktoba na
Desemba katika kalenda hiyo.
Una siku 30 katika mfululizo wake. Jina lake
limechukuliwa ktoka katika lugha ya Kilatini ‘Novem’ ikiwa na maana ya tisa.
Baada ya mabadiliko makubwa ya
kalenda ikiwamo kuongezwa kwa mwezi Januari na Februari katika kalenda ya
Kirumi ukaachwa uwepo kwenye mwendelezo wa kawaida na usomeke kama 11.
Namna mwezi
Novemba unavyoanza huwa unaanza sawa na mwezi Machi ambao ni wa mwezi wa tatu
wa kalenda ya sasa na huwa unamalizika kama mwezi Agosti kwa maana ya mwezi wa
nane.
Katika Mzingo wa Kaskazini, mwezi Novemba huwa ni mwanzo wa majira ya
baridi na katika mzingo wa Kusini mwezi huu huwa ni mwisho wa vipindi vya
baridi na mwanzo wa hali ya joto.
Aidha mwezi Novemba ni miongoni mwa miezi
mitano ambayo ina siku chini ya 31 na ni mwezi wa tano katika miezi mitano ya
mwisho.
Imetayarishwa
na Jabir Johnson……………………….Novemba 1, 2019.
Kilimo uti wa mgongo wa Tanzania
Waziri Kilimo Japhet
Hasunga akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira (kulia) na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (kushoto). Picha na Kija Elias, Moshi.
|
Kilimo ni uti wa mgongo wa
uchumi wa Tanzania. Kilimo huzalisha nusu ya uchumi wa nchi, robo tatu ya mazao
yote yanayouzwa nje ya nchi, ni tegemezi la chakula na hutoa ajira ya karibu
asilimia 80 ya Watanzania.
Licha ya sekta ya kilimo
kuaajiri watu wengi hapa nchini, mchango wa Sekta hiyo katika pato la taifa ni ndogo na watu wengi
wanaojihusisha na kilimo hasa katika
maeneo ya vijijini bado ni masikini.
Sekta hii ya kilimo ni
kubwa na ni muhimu kwa maendeleo ya taifa kwani karibu shughuli zote za
kiuchumi zinazofanywa vijijini zinategemea sekta ya kilimo.
Ripoti ya Shirika la Kilimo
Duniani (FAO) inasema mahitaji ya bidhaa za kilimo yanatarajiwa kukua kwa
asilimia 15 katika kipindi cha muongo mmoja ujao huku, ukuaji wa uzalishaji wa
bidhaa za kilimo ukitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi na kusababisha mfumuko
wa bei.
Aidha ripoti hiyo iliyotolewa
mwezi Julai mwaka huu inatoa utafiti unaolenga mwelekeo wa miaka kumi ijayo katika
soko la bidhaa za kilimo na samaki katika viwango vya kitaifa, kikanda na
kimataifa.
Katika ripoti hiyo
inaelezwa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabili wakulima katika
Mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania ni pamoja na ukosefu wa masoko ya mazao
yao ndani na nje ya nchi.
Katika miaka ya nyuma
baadhi ya wakulima wa baadhi ya mazao kadhaa
wakiwemo wakulima wa zao la kahawa waliamua kuachana kabisa na uzalishaji
wa mazao husika ikiwemo zao la Kahawa na korosho.
“Changamoto za wakulima
kukosa masoko haziwaathiri wakulima pekee, bali hata serikali hivyo ni suala
linalogusa pande zote, kwa sababu serikali nayo inategemea kupata mapato yake
kutokana na usafirishaji wa mazao nje ya nchi.
Ushelisheli yatoa wito kwa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa
Rais Danny Faure wa Ushelisheli; nchi isiyozidi watu 100,000 |
Rais Danny Faure wa
Ushelisheli amesema hakuna muda wa kutupiana lawama katika mapambano dhidi ya
mabadiliko ya hali ya hewa.
Taarifa ya Ikulu ya Ushelisheli imesema ni vema
kuacha kurushiana lawama kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Faure amesema sayansi ipo sawa katika hilo,
wanasayansi wameshazungumza kuhusu
tatizo hilo na kwamba kinachotakiwa ni hatua za kimataifa katika kupambana na
hilo na sio kunyosheana vidole vya lawama.
Faure amesema uchafuzi wa maji
katika bahari umekuwa wa kiwango cha juu kwani Kilogramu 25,750 za plastiki
zimekusanywa kutoka bahari hali inayoonyesha kuathirika kwa bahari.
Uchafuzi wa
maji katika bahari hiyo umesababisha kupanda kwa joto linalosababisha miamba
kulika. Taifa hilo la Ushelisheli linaendelea na kampeni ya kutunza maji yake na
kwamba theluthi moja ya maji yanatarajiwa kulindwa mwaka ujao katika mpango
kazi huo.
Wanasayansi wanatarajia kutoa ripoti yao kuhusu utafiti wao katika
kilele cha Mkutano wa Mabadiliko Tabia Nchi wa mataifa yaliyoko katika Bahari
ya Hindi mnamo mwaka 2022 utakaofanyika nchini humo.
CHANZO: SEYCHELLES NATION
CHANZO: SEYCHELLES NATION
Ushelisheli ni taifa la namna gani?
Ushelisheli ni taifa ambalo
ni visiwafungu katika bahari ya Hindi likiwa kiliometa 1,500 kutoka katika
Pwani ya Afrika Mashariki.
Visiwafungu vya Comoro, Madagascar, Reunion na Mauritius
vipo upande wa Kusini mwa Ushelisheli. Pia Maldives na Chagos Archipelago kwa
upande wa Mashariki. Ushelisheli ina takribani watu 94,367.
Idadi hiyo ya watu
inalifanya taifa hilo la Ushelisheli kuwa ndio
lenye idadi ndogo ya watu katika bara la Afrika. Ilijiunga na Umoja wa
Afrika baada ya kupata uhuru wake mwaka 1976.
Kutoka wakati huo hadi sasa Ushelisheli
limekuwa ni taifa linalokuwa kiuchumi likiegemea zaidi katika kilimo na utalii.
Mapema mwanzoni mwa mwaka 2010 Rais wa Taifa hilio Danny Faure alipeleka
mipango yake katika Bunge la nchi hiyo kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji
nchini humo.
Hali hiyo imelisaidia taifa hilo kuwa na uchumi bora kwani hadi
sasa ndilo taifa pekee katika bara la Afrika lenye uchumi wa juu kuliko
jingine. Hata hivyo kuwa na kiwango bora cha juu katika masuala ya uchumi
hakujafanikiwa sana kuondoa umaskini.
Mfumo wa sias ala taifa hilo ni kwamba
Rais ndiye kiongozi wa nchi na mtendaji mkuu serikali. Anachaguliwa kwa
kupigiwa kura na kukaa madarakani wa miaka mitano.
Bunge la Ushelisheli lina
wajumbe 34 huku 25 wanachaguliwa kwa kupigiwa kura kila miaka mitano.
Mfumo wa
sheria wa taifa hilo ulianzishwa mwaka 1903 ukianzisha katika mahakama ya
mwanzo hadi mahakama ya rufani. Chama kilichotawala taifa hilo ni kile cha PP
hadi mwaka 2009 kilipobadilishwa jina na SPPF.
Hata hivyo mnamo Novemba 2018
chama hicho kimebadili jina lake na kuwa Muungano wa Ushelisheli (US). Dini ya Kikristo
nchini humo ndiyo yenye wafuasi wengi ikichukua asilimia 76.2 ikifuatiwa na
Uhindu unaochukua asilimia 2.4 huku Uislamu ukishika nafasi ya tatu kwa
asilimia 1.6 ya idadi ya watu katika Ushelisheli.
Katika michezo mpira wa
kikapu ndio unaongozwa kwa kupendwa nchini humo. Tangu mwaka 2015 taifa hilo
limekuwa likipambana na mataifa makubwa kama Misri katika mchezo huo. Mji mkuu
ni Ushelisheli ni Victoria.
Imetayarishwa na Jabir Johnson………………………………Oktoba
31, 2019