Valvu za maji katika mradi wa Miwaleni-Njiapanda utakaohudumia wakazi 13,374 wa eneo hilo. |
MOSHI, KILIMANJARO
Wakazi 13,734 wa Kata ya Njiapanda
na Maeneo jirani, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wanatarajia kuondokana na
adha ya Majisafi na Salama inayowakabili, baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa
wa maji wa Miwaleni-Njiapanda ambao utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 2.3
hadi kukamilika.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na tayari serikali imeshatoa Shilingi bilioni 1. kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa
mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022, Sahir
Nyanzabara Geraruma Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
Mazingira Mjini Moshi (MUWSA), Mhandisi Kija Limbe. amesema mradi huo
utakapokamilika utaboresha hali ya huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama
katika maeneo ya Miwaleni,Mabungo na Kata ya Njia Panda.Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022, Sahir Nyanzabara Geraruma akikagua mradi wa Miwaleni
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, amesema baada ya kukagua mradi huo, amepongeza jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA), na kuwataka kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Aidha kiongozi huyo amewataka Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) kuunda Jumuiya za Watumia Maji na kuhakikisha wanazisimamia.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Njia
panda na maeneo jirani, wamesema kukamilika kwa mradi huo, kutawawezesha
kuondokana na adha ya maji, ambayo imewatesa kwa zaidi ya miaka 40.Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA), Mhandisi Kija Limbe akitoa maelezo kuhusu mradi wa Miwaleni.
0 Comments:
Post a Comment