Xinjiang maana yake ni mipaka mipya. Xinjiang ipo kwenye kona ya kaskazini-magharibi mwa China. Ilianza chini ya ukoo wa Qin maarufu kama ukoo wa Manchu kwenye karne ya 18. Imepakana na Qing Hai na Gansu kwa upande wa mashariki; Upande wa Kusini inapakana na Jimbo lililojitenga la Tibet;
Afghanistan na jimbo la Kashmir kwa upande wa Kusini Magharibi; pia Kyrgzstan, Tajikistan kwa upande wa magharibi. Kazakhstan kwa upande wa kaskazini magharibi, Russia kwa upande wa kaskazini na Mongolia kwa upande wa Kaskazini Mashariki.
Mji mkuu wa jimbo hilo ni Urumqi (Wulumqi). Kwa makadirio ya mwaka 2022, Jimbo hili lina idadi ya watu 25,852,345.
Lina maeneo muhimu kama Nyanda za Juu za Kaskazini, Bonde la Dzungarian lenye umbo la pembetatu, milima ya Tian Shan, Bonde la Tarim na safu za milima ya Kunlun.
Wenyeji wa jimbo la Xinjiang ni wakulima na wafugaji na Uighurs ndio waliokamata maeneo makubwa ya muhimu kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
Tangu kuanzishwa kwa mpango wa kuitengeneza China imara, juhudi kubwa zimewekwa kwenye jimbo hili kwa ajili ya kuuushika uchumi. Hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya watu wa jamii ya Han kuhamia huko.
Sera ya serikali ya China ni kuruhusu jamii za kikabila kuendelea na kutunza utambulisho wao wa kiutamaduni . Sera hiyo imetafsiriwa kwa mtazamo kinzani kwa kila jamii, hali ambayo imesababisha kutokea kwa mvutano mkali baina ya Uighurs na Han.
Hali ya hewa Xinjiang jangwa na misitu kwenye baadhi ya maeneo huku jimbo hilo likiwa mbali kabisa na bahari ukilinganisha na majimbo yaliyopo mashariki mwa China.
Katika maeneo ya misitu katika Xinjiang yamekuwa na mchango mkubwa kwa maisha ya watu wa China kwani uwepo wa misitu ya Tien Shan na aina za miti yanye kustahimili jangwa imekuwa kivuti kikubwa.
Takwimu za China zinaonyesha kuwa jimbo la Xinjiang imechangia pakubwa katika aina za miti muhimu kwa ajili ya tiba mbadala. Inakadiriwa kuwa aina 3,000 za miti zimegunduliwa kutoka jimbo hilo na aina 300 kutoka humo zimekuwa muhimu katika masuala ya tiba asilia.
Uighurs ni miongoni mwa jamii zaidi ya 40 zinazoishi katika jimbo la Xinjiang . Jamii kubwa inayofuatia ni Han nyingine ni kama Hui (ambao ni Wachina Waislam), Wamongolia, Wakhalka, Wakazakh, Wauzbek, Watungusic (wazungumzaji wa lugha za wamanchu na Wajibo), Watajik, Watata, na Warusi na Watahur.
Inaelezwa kati ya mwaka 1957-1967 jamii ya WaHan wapatao milioni mbili walihamia katika jimbo hilo. Wahamiaji wa jamii ya Han waliingia kwa ajili ya shughuli kiuchumi na kujikita kaskazini mwa jimbo hilo wakati wale wa Uighurs wakitokea Kusini mwa Xinjiang nao walielekea huko walipo jamii ya Han miaka ya 1980.
Asilimia 92 ya wahamiaji wa jamii ya Han iliingia jimbo humo kati ya mwaka 1950 na 1970 wakifuatiwa na jamii WaHui.
Tamaduni nyingi za Uighurs zina mizizi mikubwa kutoka katika dini ya Uislam. Uighurs na tamaduni zao wanaendelea kuwa wengi licha ya kuwa wingi wa Wachina wa Kimandarini.
Uislam nao ulikua baada ya Mapinduzi ya Kitamaduni (1960’s-1970’s) ya Mao Zedong yaliyodumu katika muongo mmoja wa mwisho wa utawala wake, hadi sasa kuna misikiti mingi iliyojengwa baada ya kipindi hicho. Pia kuna shule za kuwafundisha waislamu kuwa viongozi wa kidini wa imani hiyo.
UKOO WA HAN NEMBO YA UTAMADUNI WA CHINA
Historia ya kisiasa ya China ya zamani imekuwa na mkanganyiko mkubwa kwani baadhi ya watunza kumbukumbu wakisema koo za Xia na Shang zilitokea kwa wakati mmoja na wengine wakisisitiza kuwa kila moja ilitokea kwa wakati wake.
Wale waliounga mkono kutokea kwa koo hizo mbili kwa nyakati tofauti wanaungwa mkono na wengi kwamba ukoo wa Xia ulitawala kutoka mwaka 2070 K.W.K hadi 1600 K.W.K ukifuatia na Shang ulishika ardhi hiyo kutoka mwaka 1600 K.W.K -1046 K.W.K
Baada ya kumalizika kwa tawala hizo mbili ulikuja utawala wa ukoo wa Zhou ambao unachukuliwa kuwa ndio ulikalia ardhi hiyo kwa muda mrefu.
Ukoo wa Zhou ulitawala kwa miaka 790 kutoka kumalizika kwa ukoo wa Shang mnamo mwaka 1046 K.W.K hadi ujio wa ukoo wa Qin mnamo mwaka 256 K.W.K
Ukoo wa Qin ulitawala muda mfupi tu, wa miaka isiyozidi 20 hadi mwaka 206 K.W.K na ndio ukaaja ukoo unaochukuliwa kuwa ni fahari ya China ya sasa wa Han ambao ulishika dola hilo la mashariki ya mbali kwa miaka 426 kutoka mwaka 206 K.W.K hadi 220 B.W.K.
Licha ya kwamba zilikuja tawala nyingine nyingi hadi ukoo wa mwisho wa Qing mnamo miaka ya 1644 B.W.K hadi kuanzishwa wa China mpya na imara mnamo mwaka 1912 B.W.K ukoo wa Han bado unasalia kuwa nembo ya kiutamaduni ya China.
Ukoo huu ulianzishwa na Liu Bang ambaye alikuja kuwa mtawala wa Gaozu nakutawala kutoka mwaka 206 K.W.K hadi 195 K.W.K
Liu Bang ambaye alikuwa mnyenyekevu kwa watu wake ndiye aliyeendesha harakati za kuiangusha tawala ya Qin kwa sera zao mbovu ambazo ziliwafanya watawale muda mfupi.
Ukoo huu wa Han ulichukua mfumo wa utawala wa ukoo wa Qin na kuufanyia marekebisho kidogo yaliyowapa nguvu ya kutawala.
Waliigawanya China katika maeneo ya utawala na kuwateua maofisa watakaosimamia maeneo hayo. Hawakuishia hapo maofisa hao walikuwa wakilipwa mishahara hali iliyoweka uaminifu mkubwa kwa serikali yao.
Katika suala la imani ukoo wa Han ulichukua falsafa za Ukonfusiani (Confucianism) ambao ukoo wa Qin haukutaka suala hilo. Pia ulichukua falsafa ya Utao (Taoism)
Hata hivyo ukoo wa Han ulijiimarisha katika masuala ya kijeshi , huku ukiendelea kuteka maeneo mengi ukianzia upande wa pwani ya bahari kuelekea bara.
Katika kipindi hicho chote cha ukoo wa Han haufanikiwa kufika Xinjiang mpaka kipindi cha Mao Zedong alipoanza kuiweka China katika mfumo mwingine wa kiutamaduni.
Katika kipindi cha utawala wa ukoo huu wa Han, uvumbuzi na maendeleo makubwa yalionekana sio tu kwa ardhi ya China pekee bali duniani kwa ujumla ilikuwa chachu ya teknolojia mpya na zenye manufaa.
Kugunduliwa kwa karatasi, madaraja imara ya kamba, uchumbaji wa chumvi kwa kutumia mabomba, matoroli ya tairi moja, vinu vya kuyeyushia chuma, spana sogeza, jembe la kuvutwa na ng’ombe, rada ya kuongezea meli, kifaa cha kugundua ujio wa tetemeko la ardhi (seismograph) ni nembo ya utamaduni wa China kutoka katika ukoo wa Han.
Uvumbuzi huo ulizifanya tasnia za kilimo na afya kupata mabadiliko makubwa ambayo yaliifanya China kujijenga. Ujenzi wa Ukuta Mkubwa (Great Wall) ulikuwa zama za ukoo wa Han.
Ukoo wa Han uliifungua China katika ulimwengu mnamo mwaka 130 K.W.K kwa jamii za magharibi pale ulipoanza kufanya biashara na watu kutoka tamaduni hizo.
Kutoka kwa malengo ya kibiashara na teknolojia kulitengeneza barabara ya kibiashara iliyofahamika kwa jina la Sichou Zhi Lu ikiwa na maana ya Barabara ya Silk. Hii ilitokana na uuzaji wa bidhaa hiyo ya Silk kwa kiwango cha juu kuliko bidhaa nyingine kama vyungu.
Ukoo wa Han ulipambana vikali dhidi ya sheria ngumu za kiutamaduni zilizowekwa katika tawala zilizopita, kwani mnamo mwaka 31 B.W.K sheria iliyofahamika kwa UNIVERSAL CONSCRIPTION ilifutwa kwani kwa karne nyingi ilikuwa na madhara kwa ujenzi wa China
0 Comments:
Post a Comment