Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akiupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Steven Kigaigai katika hafla iliyofanyika Mererani wilayani Simanjiro Juni 13, 2022. |
SIMANJIRO, MANYARA
Miradi
ya Maendeleo 39 inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mkoani Manyara baada ya
kuupokea kutoka katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo utafungua, utakagua, utapitia
na kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo yenye thamani ya shilingi 23.2 bilioni
Akiwasilisha
ripoti yake wakati wa kuupokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Makongoro Nyerere amesema Mamlaka saba za serikali za mitaa zitapitiwa na
Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa katika kilometa 1200.
Mkoa
wa Manyara umeupokea Mwenge wa Uhuru leo Juni 13, 2022 kutoka mkoani
Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika viunga vya Mererani wilayani
Simanjaro.
0 Comments:
Post a Comment