Askofu Joseph Laizer wa Kanisa la Christian Life Tanzania |
Askofu Joseph Laizer wa Kanisa la Christian Life Tanzania, ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la siku tisa la Mawasiliano ya Amani (NVC) linalofanyika Kanda ya Kaskazini likijumuisha washiriki kutoka mataifa 13, kwa lengo la kujifunza namna ya kuitengeneza jamii yenye amani na utulivu kwa kuanza na maisha ya ndani ya mtu binafsi.
Amesema katika dunia ambayo maadili yameporomoka kuna ulazima wa kujifunza utu wa ndani wa binadamu ambao ndio chemichemi ya kujenga jamii iliyo bora.
Amesema kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii yamechangiwa sana na utandawazi na wazazi kukosa nafasi ya kukaa na watoto wao kwa lengo la kusema nao kwa kuwaelekeza au kuwakemea pale wanapokuwa wakifanya mambo ambayo yanaonekana kutokuwa na maadili.
"Kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii yamechangiwa sana na utandawazi lakini pia hata wazazi kukosa nafasi ya kukaa na watoto wao kwa lengo la kusema nao kwa kuwaelekeza na kuwakemea pale wanapokuwa wakifanya mambo ambayo yanaonekana kutokuwa na maadili,”amesema Askofu Laizer.
Amesema watoto wengi wanalelewa na Dada au Kaka wa kazi, hapo ndipo utakapoona kuwa mtoto anakuwa na tabia ambazo zinafanana na anayemlea na iwapo mlezi wa mtoto huyo atakuwa na tabia za hovyo ni wazi kuwa mtoto huyo atakuwa wa hovyo," amesema.
0 Comments:
Post a Comment