Wafanyakazi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWB) wakiondoa taka ngumu zinazotupwa Karibu na chanzo cha maji mto Njoro. |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti kwenye zoezi la uondoaji taka ngumu katika chanzo cha maji mto Njoro, lililoendeshwa na Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWB) wakazi hao walisema wamekuwa wakishuhudia baadhi ya wananchi wakijenga nyumba zao karibu na vyanzo vya maji ukiwemo mto Njoro, na kutirirsha majitaka kwa kuyaelekeza kwenye mto huo.
Elieneza Dhahabu
Mmbwambo, alisema kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai, kwenye maeneo
mengi ya vyanzo vya maji katika Manispaa ya Moshi,
yameathiriwa kutokana na ukame wa mara kwa mara, ikiwemo
uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo
hivyo vya maji.
Wafanyakazi wa bonde la Pangani, kuzoa taka ngumu kutoka chanzo cha maji mto Njoro. |
“Wako baadhi ya akina
mama ambao hawataki kulea watoto wao, wanapojifungua wamekuwa wakija nyakati za
usiku na kutupa vichanga vyao katika mto huu, huku wengine wamekuwa wakija
kutupa hata mizoga ya mbwa pamoja na uchafu wa kila aina wakijua kwamba eneo
hilo ni sehemu salama, ,”alisema Mmbwambo.
Mmbwambo alisema
uchafuzi huo umeendelea kuongezeka kwa kasi na kuathiri maji, hewa pamoja na
ardhi na hivyo kuhatarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla
wake.
“Juzi tumekuta
kuna kitoto kichanga kimetupwa katika mto huu, tukapiga simu polisi
ambapo walikuja na kukiondoa kichanga hicho kikiwa tayari
kimeshafariki na wanawake hawa wamekuwa wakitupa nyakati za usiku watu wakiwa
wamelala,”alisema.
Mkazi wa Njoro Alawi Jumanne, alisema wengi wanaotupa taka taka na kutiririsha maji katika mto huo ni wale ambao wanaishi karibu na chanzo vyanzo vya maji, kwani wengi wao hawataki kuchangia gharama za kulipia maji taka Mamlaka ya Maji safi na Mazingira mjini Moshi (MUWSA) na hivyo kuamua kuelekeza uchafu huo kwenye mto hiyo.
Kwa upande wake
Mhandisi Selemani Mdee kutoka Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWB), aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha wa kuwatolea taarifa wananchi
wanaojihusisha na shughuli za uchafuzi wa mazingira katika mito na vyanzo vya
maji ikiwemo utupaji taka, ili watu hao waweze kukamatwa na kufikishwa katika
vyombo vya kisheria.
“Unapotupa taka ngumu
kwenye vyanzo vya maji, zingine zinakuwa na kemikali zenye sumu ndani yake,
hivyo nitoe wito kwa wananchi kutokutupa taka taka katika vyanzo vya maji,
lakini pia kutokujenga makazi karibu na vyanzo vya maji,”alisema Injinia Mdee.
Alisema katika zoezi hilo la uondoshaji taka ngumu zilizokuwa zimetupwa katika mto Njoro zaidi ya tani mbili waliweza kuziondoa na kwamba kama taka taka hizo zingeendelea kuwemo katika mto huo viumbe maji wangeweza kufa lakini pia hata viumbe hai wengine wangeweza kupotea kabisa duniani.
Naye Mtaalamu wa maji
Juu ya Ardhi Mhandisi Anna Kiondo, aliwataka wananchi kuzingatia Sheria ya
Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye
maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60.
“Tunawataka
wananchi kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya
mwaka 2009 kifungu cha 11 ambayo inapiga marufuku wananchi kufanya
shughuli zozote za kibinadamu zenye kuhatarisha usalama wa maji na uchafuzi wa
mazingira kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji,”alisema Injinia Kiondo.
Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka
mara nyingi amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari, akiwataka wananchi na
jamii kwa ujumla wake kuheshimu sheria ya mazingira hasa kufanya ujenzi ndani
ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji, kwani maeneo ya mito na mabonde kisheria ni
maeneo yanayo milikiwa na bonde la maji ambao wao wanawajibika kuhakikisha
ustawi wa mazingira katika maeneo hayo.
Dkt. Gwamaka amesema
kuwa sasa hivi kumetokea tatizo la wananchi kujenga ndani ya mita 60 kutoka
vyanzo vya maji ambayo kisheria ni makosa makubwa. Hata hivyo ujenzi wa ndani
ya mita sitini husababisha athari kubwa sana kwa wananchi wenyewe na
kimazingira.
“Kutokana na athari
kubwa zinazojitokeza sisi kama Taasisi tunaendelea kuelimisha jamii kuwa
kujenga ndani ya mita sitini unajiweka katika eneo hatarishi kwa mafuriko.
Mbali na hayo mafuriko kama sasa hivi kumekuwa na tatizo la watu kutupa taka
ndani ya mito, hivyo utakuwa sehemu ya dampo na hata ustawi wa mazingira
unaharibika kwa ujumla wake”
Ameendelea kusisitiza
kuwa ustawi wa mazingira una haribika kwa mfano katika maeneo ya bahari tunaustawi
mkubwa sana wa mikoko ambayo ni hazina ya Taifa ambayo hutakiwi kuikata kwa
sheria ya misitu kwa maana hiyo katika maeneo kama hayo hutakiwi kujenga wala
kuendeleza kitu chochote
“Sisi kama Baraza
tunachukua hatua hasa tunapogundua mwananchi amejenga ndani ya maeneo ya mikoko
na kunabaadhi wameshitakiwa ambao wamejenga ndani ya mikoko lakini kubwa zaidi
ni kuelimisha wananchi, sehemu kubwa ya wananchi hawaelewi hizi sheria sasa
Baraza lipokwenye mkakati wa kuhakikisha kwamba kupitia.
0 Comments:
Post a Comment