Saturday, June 11, 2022

Ngamia katika mbuga za Kikafu Soka-Kimashuku

 

Ngamia ni mnyama mwenye nundu mgongoni na hutumiwa kusafirisha watu na mizigo. Wengi hupatikana katika bara la Afrika na Asia kutokana na mazingira yake ya ukame na jangwa.

Mambo yamebadilika hata nchini Tanzania unaweza kuwapata wanyama hawa katika maeneo yenye ukame na mvua chache kwa mwaka.

Hai ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro, lakini suala la ngamia limekuwa mojawapo ya shughuli zinazofanywa na watu wa maeneo hayo.

Ngamia waliingia katika maeneo hayo kutoka na ujio wa Wasomali wengi kutoka nchini Kenya na Somalia na kuweka makazi.

Vijana wa Kitanzania wamekuwa wakipata ajira ya uchugaji wa wanyama hao.

Watanzania wengi wanapomtazama ngamia humuona kama kiumbe wa ajabu hivyo suala la picha wakiwaona wanyama hao ni jambo la kawaida kabisa kuwakuta wakipiga picha.

Kama inavyoonekana pichani ni katika mbuga za Kikafu Soka zilizopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kama JAIZMELA  ilivyowakuta wanyama hao wakipata malisho.

Watu mbalimbali hupendelea kupiga nao picha pindi wanapowaona ngamia. Kama ambavyo inaonekana katika picha ni Maria A. Mbasha mkazi wa Kijiji cha Kimashuku wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.



MAISHA YA NGAMIA YAKOJE?

Maisha ya ngamia ni kati ya miaka 40 mpaka 50, kimsingi ngamia wapo wa aina Mbili, mwenye nundu moja ndio maarufu sana hapa Afrika, wakati aina ya pili ambao hubeba nundu mbili na vinyweleo vingi wakipatikana huko Asia, waone na miili yao vile vile na mwendo wao wa taratibu lakini ukitaka kumharakisha yawezekana pia, akishika njia hukimbia kilometa 40 na zaidi kwa saa moja tu ambao ni kasi ya mwendo wa baiskeli.

Kwa urefu huwa na futi 6 mpaka 7, na uzito wao ukicheza kati ya kg 300 mpaka 1000 endapo matunzo mazuri atapewa,

Mtoto wa ngamia hupevuka anapotimiza miaka 7, Ngamia jike ni kiumbe ambaye kwa mapozi na maringo amebobea, humzungusha sana dume pindi anapotaka wastarehe, mpaka jike akubali na kujilaza chini dume hutumia mbinu nyingi sana, ikiwa ni pamoja na kimlamba, kumchezea shingo, kumkuna na anapokuwa mkaidi dume huchukia na kumuuma kabisa, hapo jike ndio kidogo atamfikiria.

Ngamia ni mtulivu, na nidhamu ya hali ya juu. Ngamia ni mstahimilivu sana katika mazingira ya ukame, anaweza akadumu kwa muda mrefu sana pasipo ya kula wala kunywa.

Siri ya kuwa hivyo ni ile nundu aliyonayo pale juu, huweza kubeba kiasi kingi cha wanga kinachomsaidia kujimudu anapokuwa katika mazingira kama hayo, hunywa maji zaidi ya lita 110 na si mwepesi kupata kiu.



0 Comments:

Post a Comment