Wafanyabiashara wa soko la Chekereni wakijiandaa kuondoka baada ya kufanya manunuzi Juni 14, 2022 |
Kila
aina ya usafiri duniani inaongozwa na sheria za jumla na sheria mahususi kwa
usafiri huo.
Barabarani
ni kama kijijini, watu walioko katika kijiji hicho lazima wawe na mahusiano
mema.
Kama
ilivyo kijijini, barabarani nako kuna waendesha mikokoteni, wanyama, wachungaji
wa wanyama, waendesha bodaboda, madereva wa magari, watembea kwa miguu, wajenzi
na wakarabati wa barabara, wasafishaji, abiria, n.k
Wote
wana haki ya kutumia barabara. Kimsingi hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine
barabarani, wala barabara hazikujengwa kwaajili ya vyombo vya moto tu, au
magari peke yake.
Sote
tuna haki na ili tutembee salama na kwa amani ni lazima ziwepo taratibu za
kutuongoza.
Unaweza
kuuta usafiri kafiri, lakini inawalazimu wasafiri wa kutumia kutokana na sababu
mbalimbali.
Wafanyabiashara
wa soko la Chekereni wanaofanya biashara zao na kuzipeleka maeneo mbalimbali ya
karibu ikiwamo Himo mjini Moshi hawana ujanja zaidi ya kutumia usafiri huo
(kama inavyoonekana kwenye picha iliyopigwa na Kija Elias Juni 14, 2022).
0 Comments:
Post a Comment