Friday, June 10, 2022

MAKTABA YA JAIZMELA: Vita iliyotumia muda mfupi zaidi kupiganwa

 


Katika zama zote tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia vita imekuwa ni mada muhimu ya kujadiliwa na kufanyiwa uchambuzi wa kina.

Katika karne ya 20, vita kubwa zaidi kutokea dunia ni pale mataifa mbalimbali yalipoingia kupigana na kutengeneza kile kinachofahamika hadi sasa kama vita ya kwanza na ya pili ya dunia.

Vita hizi mbili zilipigwa kwa misingi ya zana kali za kivita ikiwamo mabomu ya nyuklia, kibaolojia na mauaji ya kemikali vyote hivyo vilitumika kutafuta ushindi kwa kila upande ulioshiriki.

Kuelewa ziaidi kuhusu asili ya vita ni mjadala mrefu lakini kwa ufupi ni kwamba vita zimesaidia sana kujua matarajio ya binadamu katika siku za usoni pia kujua tabia ya binadamu.

Vita zimetokea nyingi na kuweka rekodi mbalimbali. Hata hivyo kuna vita ambayo imeingia katika rekodi kwa kupiganwa muda mfupi zaidi duniani, unaifahamu? Kaa kwa kutulia ni hii

ANGLO-ZANZIBAR

Hii ilikuwa vita baina ya Waingereza na Waarabu katika kisiwa cha Unguja ambayo ilipiganwa kwa dakika 38 na kumalizika.

Vita hii ilitokana na kifo cha ghafla cha Sultan wa Zanzibar. Binamu wa Sultan alijitangaza kuwa ndiyo mtawala mpya jambo ambalo lilipingwa na utawala wa Waingereza. Vita hiyo ilipiganwa Agosti 27, 1896.

Mtawala wa Waingereza alitaka kila mtawala mpya lazima apitie uhakiki ambao utafanywa na waingereza.

Khalid bin Barghash aliamua kukusanya wanajeshi wake 2,800 katika ofisi za Waingereza. Waingereza nao waliamua kuweka majeshi yao hapo ikiwamo mizinga miwili, meli 150 na wapiga mbizi na wanajeshi 900 wa Kizanzibari.

Kilimchomshinda Barghash alikuwa na silaha chache na zenye uwezo mdomo (handful of Maxim guns, a Gatling gun, a 17th-century bronze cannon and two 12-pounder field guns).

Saa mbili za asubuhi ya Agosti 27, 1896 alitaka wakutane na utawala wa Kiingereza lakini waingereza waligoma kuketi chini na kuzungumza. Saa moja na dakika mbili baadaye waingereza walirusha mizinga yao na kuwatawanya wafuasi wa Barghash.

Saa 3:40 asubuhi vita hiyo ilimalizika na Barghash alisalimu amri. Wafuasi wake 500 walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika vita hiyo huku Mwingereza mmoja tu akijeruhiwa katika vita hiyo fupi duniani.

Barghash alikimbilia kwa Wajerumani  na baadaye uhamishoni. Mchana wa siku hiyo hiyo Waingereza walimsimika sultan mpya wa Zanzibar.

 

0 Comments:

Post a Comment