Monday, June 6, 2022

Kilimanjaro yaupokea Mwenge wa Uhuru leo

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai (kushoto) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Kigoma Malima katika hafla iliyofanyika kwenye kijiji cha Bendera wilayani Same mkoani Kilimanjaro mnamo Juni 6, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai ameupokea Mwenge wa Uhuru leo katika hafla iliyofanyika kwenye kijiji cha Bendera wilayani Same mkoani hapa.

Kigaigai ameupokea mwenge huo ukitokea Tanga kwa Mkuu wa Mkoa Adam Kigoma Malima ulikokimbizwa kwa siku 11 na kuzindua miradi 82 yenye thamani ya shilingi bilioni 33.

Mkoani Kilimanjaro utazunguka kwa siku saba ukianzia Same ambako utazindua miradi 38 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 13.

Utazunguka kwa takribani kilometa 800, ukikimbizwa na Mkimbiza Mwenge kitaifa mwaka huu Sahir Nyanzabara Geraruma akiwa na wenzake watano.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Sensa ni Misingi wa Mipango ya Maendeleo: Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa.






0 Comments:

Post a Comment