Tuesday, June 28, 2022

China itakubali Xinjiang kujitenga kama Tibet?

 

Kuna taarifa zinaelezwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kinachoendelea nchini China katika jimbo la Xinjiang ambapo serikali ya nchi hiyo chini ya Xi Jinping imebainika kuwatesa kikatili watu wa kabila la Uighurs.

Hayo yalibainika baada ya kuibiwa kwa taarifa za kiintelenjisia  zikiwaonyesha askari wa China wakiwatesa vikali watu wa Uighurs na wengine wakitupwa jela kwa makosa ya kuonewa.

Serikali ya China imekanusha madai hayo huku mataifa ya magharibi yakiendelea kupigilia msumari wa moto kuwa inatenda jinai zisizomithirika kwa watu wa jamii hiyo.

Hata hivyo kuna maswali mengi kuhusu kudhibitiwa kwa Uighurs katika jimbo hilo lakini pia mengine yanajitokeza kwanini mataifa ya magharibi yamekuwa mstari wa mbele kuitetea jamii hiyo yenye idadi kubwa ya watu ikifuatiwa na Han.

Wachambuzi wa masuala ya jamii na siasa wamekuwa wakitofautiana kuhusu udhibiti wa Uighurs ambao umekuwa utambulisho wa Jimbo la Xinjiang.

Utaikumbuka kazi nzuri ya mke wa Mao Zedong aliyefahamika kwa jina la Jiang Qing, Waziri wa Ulinzi Lin Biao, msaidizi wa muda mrefu wa Mao ndugu Chen Boda ambaye akiwa na wenzake Kang Sheng na Wang Dongxing katika masuala ya usalama pia Waziri Mkuu Zhou Enlai walivyomuunga mkono Mao katika kuhakikisha China inasisimama licha ya vurugu za hapa na pale.

XINJIANG ITAJITENGA?

Kinachojitokeza kwa sasa ni madai ya Xinjiang kutaka kujitenga kama ilivyofanya Tibet,. Xinjiang  inazidisha mshtuko zaidi kwa China ya sasa kwani idadi ya majimbo yatakayotaka kujitenga inaweza kuzidi. Hebu fikiria kwa kivumbi cha China bara na Hong Kong kilivyo huku Beijing ikisisitiza haitaiachia Hong Kong.

Tibet ni wafuasi wa Ubudha na imekuwa alama yao, Xinjiang itaweza kuziweka imani zote mbili katika eneo hilo ya Uislam inayofuatwa na Uighurs na Ukonfusiani unaoaminiwa na jamii ya Han ambayo ina mizizi mikubwa katika ardhi ya China?

KWANINI CHINA HAITAKUBALI XINJIANG IKALIWE NA UISLAM

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakiilenga China kama tishio lao katika kila nyanja hususani uchumi hivyo kelele katika udhibiti wa Uighurs ambao kwa asili wanaingilia na lafudhi za Kituruki.

China kuwaruhusu Uighurs kutanuka ni kuruhusu tamaduni za magharibi kuingia katika ardhi hiyo na kuharibu taratibu zao zilizojengwa kwa muda mrefu na kuitambulisha China duniani.

Xi atakuwa amejifunza kutoka kwa waliopita namna walivyoweza kuulinda utamaduni wa China dhidi ya tamaduni nyingine katika ardhi hiyo, hivyo wanachotendea Uighurs ni kwa maslahi ya China na sio vinginevyo.

Kama ambavyo tumekuwa tukiona taifa kama Marekani linavyojinasibu katika mienendo yake kuwa kinachofanyika ni kwa maslahi ya Marekani, ikiwa na maana unapoliona taifa hilo likiingilia masuala ya nje ni kwa maslahi yake na sio kwa hao wanaonyanyaswa.

Mao Zedong, mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Kikomunisti  (CCP) alishtuka mienendo ya Usovieti hadi anguko lake hivyo kuamua kwa moyo mmoja kuanzisha njia nyingine ya kuiimarisha China kwa gharama yoyote maadam China isianguke.

Ndivyo ilivyo kwa Xi ambaye naye ni mwenyekiti wa maisha wa CCP, kwa gharama yoyote hawezi kuwaacha Uighurs waharibu utamaduni wa ukoo wa kihistoria wa Han ambao umewafikisha hapo walipo.

Picha ya kuchora ikionyesha namna wafungwa katika mojawapo za jela kwenye jimbo la Xinjiang.

 

0 Comments:

Post a Comment