Imeelezwa
kuwa chini ya asilimia 30 ya watanzania nchini ndiyo wanaofahamu huduma za
msaada wa kisheria.
Utafiti huo umefanywa na Taasisi inayowezesha azaki zinazotoa huduma za wasaidizi wa kisheria nchini ya Legal Service Facilities (LSF).
Akitoa taarifa hiyo katika mafunzo ya siku moja ya wanahabari kanda ya kaskazini yaliyofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro Meneja Mawasiliano wa LSF Jane Matinde amesema idadi hiyo imetokana na uelewa mdogo wa jamii katika masuala ya kisheria.
Pia amesema jiografia ya baadhi ya maeneo nchini imekuwa ikichangia kiasi kikubwa cha wasaidizi wa masuala ya kisheria kutowafikia wananchi.
Matinde ameongeza kuwa LSF imewezesha mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria 4,000 kutokana na changamoto mbalimbali za kijamii ikiwamo kuhama makazi imesababisha kupungua kufikia 3,000.
LSF ilianzishwa mwaka 2011 kama shirika lisilo la kiserikali linalopokea ruzuku kutoka kwa wafadhili na kuwezesha mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.

0 Comments:
Post a Comment