Historia
ya mimea na viungo imekuwa tangu mwanzo wa nyakati za binadamu, hii ikiwa na
maana kabla hata ya matukio kuanza kurekodiwa, Wamisri wa mwanzo walikuwa wakihifadhi
miili ya marehemu zao kwa mimea na viungo.
Ulaya iliingia katika kuuza viungo
hivyo kupitia vita mbalimbali ambako kulikuwa na uhitaji mkubwa wa viungo
hivyo. Makabrasha yaliyohifadhiwa yanaonyesha mdalasini ulikuwa maarufu sana
katika Kusini Mashariki mwa Asia, China na sio Misri.
Hata hivyo biashara ya viungo inaonyesha ilianza kufanya miaka 3,500 iliyopita. Kuanzia mwaka 950 K.K Wafanyabiashara wa Kiarabu walianza kufanya biashara kwenda India, China na Kusini Mashariki mwa Asia kwa kutumia punda na ngamia kwa ajili ya kuchukua viungo. Lakini madhumuni makubwa yalikuwa sio matumizi yao wenyewe bali ni kuwapelekea Wagiriki.
Wakati Alexander the Great akiivamia Misri mwaka 80 K.K alianzisha bandari ya Alexandria ikiwa ni maalum kwa biashara ya viungo. Iliingia barani Ulaya kwa namna hiyo ambapo Warumi wa kale walitumia viungo katika chakula, dawa na kuondoa harufu mwilini kama pafyumu. Na kipindi hicho shehena kubwa ya dhahabu na fedha ilibadilishwa kwa viungo.
Baada ya karne ya kwanza Warumi walianza kwenda moja kwa moja India kupitia bahari ya Shamu hivyo kumaliza umiliki wa muda mrefu wa waarabu katika biashara hiyo. Ushahidi unaonesha kuwa wakati Goths ambao walikuwa wakiishi katika pembezoni mwa mto Danube walipoivamia Rome mwaka 410 walichukua shehena kubwa ya dhahabu, fedha, hariri na kilo 1300 za pilipili ili kuweza kutoweza kuwaua warumi.
Hivyo unaweza kuona namna viungo vilivyokuwa na thamani. Ukaapita muda mrefu mpaka karne ya 14 ilipoanza tena, upelelezi kupitia bahari uliboreshwa Zaidi ikilinganishwa na karne nyingi nyuma. Biashara ya viungo ikaanza kushamiri tena ambapo mwaka 1492 Christopher Columbus alivumbua New World.
Kutoka mwaka 1519 hadi 1522 Hispania walipata njia hadi katika kisiwa kinachofahamika kama Spice (Moluccas) karibu na Indonesia ambako karafuu, komamanga na pilipili vilikuwa vikistawi sana. Waliokuwa wakimiliki viungo na mimea yake walikuwa ndiyo matajiri wa siku.
Ilipofika mwaka 1800 mashamba makubwa yalianzishwa na maeneo mengine ulimwenguni hivyo kusababisha biashara ya viungo kukosa nguvu kutokana na ulimaji huo. Hakukuwa na haja tena ya kwenda India kufuata viungo. Kutoka mwaka 1990 hadi 1994 rekodi zinaonyesha nchi ya Marekani iliingia kiasi cha Shilingi bilioni 850 zinazotokana na viungo.

0 Comments:
Post a Comment