Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James akihutubia katika Uzinduzi wa Mkakati wa 'Kilimanjaro Ya Kijani' Juni 16, 2019. |
Akizungumza na viongozi wa
Mabaraza ya kata kutoka wilaya za Mwanga, Rombo, Moshi Vijijini, Same , Siha,
Moshi mjini na Hai, wakati wa uzinduzi
wa daftari la wanachama wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za CCM mkoa; Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri James, alisema
vijana wanapaswa kuwa waaminifu ili waweze kushinda wakati wa uchaguzi.
Akisisitiza alisema mara nyingi wamekuwa wakishindwa
katika baadhi ya chaguzi zilizowahi kutokea katika baadhi ya majimbo ni
kutokana na kutokuwepo kwa umoja na mshikamano kati ya viongozi na wana chama
wa chama hicho.
James alifafanua kuwa ili
chama kiendelee kushika dola ni muhimu kwa Wana CCM kuacha tabia za chuki,
fitina, malumbano na kupakana matope
kwani wao ni familia moja hivyo ni vyema wakaendelea kuwa wamoja ili kuweza
kukijenga chama.
Mwenyekiti huyo pia alizindua
mkakati unaojulikana kama “Kilimanjaro ya Kijani” ambayo imelenga kuwaandaa vijana wa CCM kuelewa na
kutambua hali halisi ya kisiasa mkoani humo.
STORY & PHOTO BY: Kija Elias and Jabir Johnson
Wanachama wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro katika mkutano wao Juni 16, 2019 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano CCM Mkoa wa Kilimanjaro |
0 Comments:
Post a Comment