Thursday, June 6, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Sukarno-Mwasisi wa Taifa la Indonesia


Sukarno alikuwa kiongozi wa kwanza wa Indonesia ambaye alipambana kuipatia uhuru nchi hiyo. 

Alizaliwa Juni 6, 1901katika Java wakati kisiwa hicho kilipokuwa mali ya Dutch East Indies, Sukarno aliibuka na kuwa mwenye nguvu mwaka 1949. 

Sukarno badala ya kuunga mkono mfumo wa asili wa bunge na aliunda mfumo mwingine wa kidemokrasi lakini ukiwa mikononi mwake. Mwaka 1965 Sukarno aliondolewa kwa nguvu za kijeshi na ukawa mwisho wake wa kukalia kiti cha kuliongoza taifa hilo. 


Alifariki dunia akiwa nyumbani kwake Juni 21, 1970 mjini Jakarta. Sifa yake kubwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu  pia alikuwa na kipaji cha kuzijua lugha ikiwamo Kijava, Kibali, Kisunda, Kiholanzi, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kibahasa cha Indonesia, Kijerumani na Kijapan. 

0 Comments:

Post a Comment