Friday, June 7, 2019

Chadema yashauriwa isishiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na 2020


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshauriwa kususia chaguzi zote zinazofanyika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwemo ule wa Serikali za Mitaa na uchaguzi  mkuu wa mwaka 2020. 

Ushauri huo ulitolewa jana na diwani  mteule wa Kata ya Uru Shimbwe Bertin Mkami, wakati wa zoezi la kukabidhiwa barua za uteuzi wake, baada ya kupita bila kupingwa  na kutangazwa jana na Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Kastory Msigala, ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini. 

Mkami alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)nchini Tanzania,  kilitangaza kususia uchaguzi wote mdogo wa Ubunge na udiwani, hivyo nina kishauri chama hicho pia  kisusie hata uchaguzi wa serikali za Mitaa  unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na  ule wa mwaka 2020. 
Deogratius Mushi
 “Kama wataendelea kususia  zaidi na  mwaka 2020 kwenye uchaguzi mkuu nawaomba wasuse zaidi, ili sisi tuendelee tuitekeleze Ilani yetu ya CCM, hata kama wataendelea kususia sisi tutaendelea kuitekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo zaidi ,”alisema Mkami. 

Kwa upande wake Diwani mteule wa Kata ya Kibosho Magharibi Deogratius Mushi, alisema wataendelea kumuunga mkono rais Dkt John Magufuli katika harakati zake zote za kuwaletea wananchi maendeleo. 

Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi, kwenye mkutano wa kuwashukuru kwa  kupita bila kupingwa , uliofanyika katika soko la Mawaleni Mushi, aliwahakikishia wananchi hao kuwa atahakikisha ahadi zake zote alizoziahidi za kuwaletea wananchi maendeleo anazitekeleza kwa vitendo. 

Mushi alisema ahadi alizozitoa mwaka wa 2015  wakati wa kuwaomba ridhaa wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi ni pamoja na miradi ya usambazaji umeme, maji, ujenzi wa baraba kwa kiwango cha lami na moramu  pamoja na ununuzi wa gari la kubebea wagonjwa, ambapo kwa kuwa ndani ya CCM miradi hiyo itatekelezwa kwa kushirikiana na serikali inayoongozwa na Dkt Magufuli. 

Vilevile aliwahakikishia  kuwa changamoto ya  soko la Mawaleni, inayowakabili wafanyabiashara wadogo wadogo, linafanyiwa ukarabati, ambapo alisema atahakikisha anajenga vizimba na kuweka bati kwa ajili ya kijikinga na jua pindi wanapofanya biashara zao.

STORY & PHOTO BY: Kija Elias

0 Comments:

Post a Comment