Sheria ya mitandao iliyoaanza kutumika rasmi Septemba 1, 2015. Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa
kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao
2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi
wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia
mitandao
3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama
zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook,
YouTube, Instagram n.k)
4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa
kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii
5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya
vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu
6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya
simu utakugharimu
7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika
kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu
8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha
watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu
9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga
mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia
hatarini
10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand'
ama jina la mtu itakugharimu
HUKUMU
Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha
isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika (au vyote!)
CHANZO: MICHUZI BLOG
0 Comments:
Post a Comment