Unaweza kufikiri utani kwa kijana huyu mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkazi wa mkoani Mbeya ambaye kwa moyo wake wa dhati ameamua kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutembea kwa miguu kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Kwa sasa yupo mkoa wa
10 tangu aanze mwezi Mei mwaka huu. Anafahamika kwa jina la Ramadhani Salum
Mohamed alizaliwa Juni 6, 1989 Masasi mkoani Mtwara. Alianza safari yake mjini
Gairo akitokea Mbeya.
Ana simulizi ya kustaajabisha sana. Lakini kubwa Zaidi ni
kwamba kila anapofika katika kijiji, mji au mkoa hupita katika ngazi za utawala
zinazotambulika ikiwamo polisi, maofisa watendaji wa vijiji na kata.
Kwa ufupi tu huyu ndiye aliyetembea kwa mguu
kutoka Mbeya hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuiunga mkono timu yake ya Simba
SC baada ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambapo katika
msimu wa 2018/19 ilitinga robo fainali ya mashindano hayo makubwa barani Afrika
katika ngazi ya vilabu.
STORY BY: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment