Saturday, June 8, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Unamkumbuka Suharto, Rais wa Pili wa Indonesia?




Suharto ni rais wa pili wa taifa la Indonesia. Alizaliwa Juni 8, 1921 katika kijiji cha Kemusuk kilichokuwa katika dola ya Yogyakarta. Suharto alizaliwa wakati wa utawala wa Wadachi katika Indonesia wakati huo ikiitwa Dutch East Indies. 

Alizaliwa katika familia maskini iliyokuwa ikiishi katika nyumba iliyojengwa kwa miti ya mianzi na kusilibwa na udongo katika ardhi ya Wajava. Kiongozi huyo wa kijeshi aliingia madarakani  baada ya kumtoa madarakani Sukarno ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo. 

Alianza kushikilia hatamu tangu mwaka 1967 hadi alipojiuzulu mwaka 1998. Katika hotuba yake ya kujiuzulu aliowaomba radhi watu wa Indonesia kwa makosa ambayo aliyafanya wakati wa utawala wake.


Suharto alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kemusuk karibu na jiji la Yogyakarta. Alikuwa katika hali ya unyenyekevu. Wazazi wake wa Kijava waliokuwa waumini wa dini ya Kiislamu walitalikiana na kusalia kama wadaawa muda mfupi baada ya Suharto kuzaliwa. 

Wakati wa utawala wa Wajapani katika Indonesia, Suharto alihudumu katika Jeshi la Ulinzi la Wajapan. Wakati wa harakati za kupata uhuru kwa taifa hilo alikuwamo katika Majeshi ya Indonesia. Suharto alifanikiwa kupanda cheo na kuwa Meja Jenerali baada ya Uhuru wa Indonesia. Alifanya jaribio la kupindua utawala wa Sukarno (mwasisi wa taifa hilo) na kufanikiwa Septemba 30, 1965 akiungwa mkono na Chama cha Kikomunisti cha Indonesia. Aliteuliwa kushika nafasi ya urais baada ya jaribio hilo mwaka 1967 na mwaka 1968 alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo. 

Aliposhika madaraka hiyo alianza kuongoza taifa hilo kwa kuweka sheria ambazo zilikuwa zikimpa kuitambulika na raia wa taifa hilo. Suharto alikuwa imara miaka ile ya 1970 hadi 1980. Mwanzoni mwa miaka ya 1990  hali ilikuwa mbaya katika taifa hilo, ambalo inaelezwa udikteta ulitawala  na vitendo vya rushwa. Hali hiyo ilimlazimisha kujiuzulu May 1998. 

Wakati wa kujiuzulu kwake aliomba msamaha kwa Waindonesia wote kwa yaliyotokea kwani yalisababisha uchumi wa taifa hilo kubaki nyuma. Suharto alifariki dunia jijini Jakarta, Indonesia Januari 27, 2008 akiwa na umri wa miaka 86. Suharto alizikwa kitaifa. 

0 Comments:

Post a Comment