Saturday, June 1, 2019

UTAFITI: Binadamu anapaswa kunywa lita 200 za maziwa kwa mwaka

Chama cha Wasindikaji Maziwa Tanzania (TAMPA) kimesema mtu mmoja mzima anatakiwa kunywa lita 200 za maziwa kwa mwaka. 

Hata hivyo hali halisi nchini Tanzania inaonyesha ni mtanzania anaweza kunywa chini ya lita mia moja kwa mwaka kiwango ambacho ni kidogo. . 

Jukwaa la maziwa  la Mkoa wa Kilimanjaro limesema uzalishaji wa maziwa wa maziwa Dkt. Anna Mgwira umekuwa ni lita 5 hadi 8 kwa siku. 

Kwa upande wake mkoa wa Kilimanjaro amewataka watanzania  kunywa maziwa kwa kiwango ambacho kimetajwa.   

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amewataka watanzania  kuacha tabia ya kutorosha maziwa kwenda nje ya nchi kutokana na ukweli kwamba mchezo huo ukiendelea maziwa yatakuwa adimu hivyo uwiano wa lita 200 itakuwa kitendawili. Na kuongeza kwamba lishe ya mtanzania itaathirika.
Mkurugenzi wa KDCJE Nancy Kidin akizungumza na vyombo vya habari katika siku ya kuhamsisha unywaji maziwa mkoani Kilimanjaro.


0 Comments:

Post a Comment