Friday, June 14, 2019

Kandambili zina maana gani kwa Mtanzania?



Juni 14 kila mwaka dunia inaadhimisha siku kandambili. Nchini Tanzania zinaonekana kuwa ni aina ya bidhaa inayodharaulika. 


Mbali na kudharaulika bidhaa hiyo imekuwa ikizalishwa kwa wingi. Jaizmela News imezungumza na watanzania baadhi kuhusu matumizi ya bidhaa hiyo; mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Aisha anasema, “Ninavyojua kandambili tunazitumia kwa kuogea, pindi ambapo ninakwenda kuoga tu.” 

Tafsiri inayoonekana mtu yeyote anayevaa kandambili katika kazi zake za kila siku ikiwamo kwenda nazo katika kazi zake za kujiajiri huonekana mshamba au mwenye shida. 

Aidha kijana wa kiume aliyejitambulisha kwa jina la Omary Suleiman anasema, “Sio ustaarabu kuvaa kandambili katika mizunguko ya maisha, ibakie kandambili kuwa ya kuogea. Mitazamo kuhusu kandambili umeendelea kuwa tofauti, Richard Teveli wa Majengo mjini Moshi anasema uchumi wa watanzania upo tofauti kwani kuna wengine wanauwezo wa kununua kandambili suala la kwamba inatumika kuogea pekee ni jambo ambalo limezoeleka. 

“Kuna wengine hawana hata pesa za kununua kiatu, isitoshe kandambili zinauzwa kwa bei rahisi na upatikanaji wake ni mwepesi kutokana na uzalishaji wake, nashauri kandambili muhimu. 

Wengine wanasema kandambili ni nzuri kuzitumia kutokana na kwamba hawawezi kuvaa viatu muda wote, hivyo wanatumia kandambili ili miguu ipate ahueni (ipoe) Je ni kweli kwamba kandambili zinatengenezwa kuwa ni kwa ajili ya kuogea.

Historia ya Kandambili (Flip-Flop)
Mgahawa wa vinywaji laini wa Tropical Smoothie uliopo Atalanta, Georgia nchini Marekani miaka 10 baada ya kuanzishwa kwake ulikuja na wazo la matumizi ya kandambili. 

Hiyo ilikuwa mwaka 2007 wakati mgahawa huo ulioanzishwa Casco, Maine nchini humo ulipokuwa ukisherekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake. Wateja walitakiwa kuvaa kandambili ili waweze kupokea juisi yenye mchanganyiko wa ndizi na strawberry maarufu nchini humo kwa jina la Jetty Punch Smoothie. 

Aidha Tropical Smoothie waliwapa wateja wao kandambili za karatasi ili waweze kuwapelekea watoto waliokuwa wagonjwa na familia zao zilizokuwapo maeneo ya Camp Sunshine. Kandambili hizo za karatasi zilikuwa zikimgharimu mteja dola moja Marekani. 

Mnamo mwaka 2015 Tropical Smoothie Café ilifanya changizo la dola za Kimarekani Milioni Moja kwa ajili ya Camp Sunshine. Na utaratibu huo wamekuwa nao kwa ajili ya kuchangia Camp Sunshine.

0 Comments:

Post a Comment