Jina
lake halisi ni Raúl Modesto Castro Ruz alizaliwa Julai 3, 1931 katika kijiji
cha Birán nchini Cuba, mwana wa baba wa Uhamiaji wa Hispania, Ángel Castro, na
mama mzaliwa wa Cuba wa uzazi wa Canarian, Lina Ruz.
Katika kijiji cha Biran baba yake alikuwa
mmiliki wa mashamba makubwa inaelezwa alikuwa akimiliki ekari 23,000. Raúl ni
mdogo zaidi kwa ndugu watatu: Ramón, Fidel na yeye mwenyewe. Pia ana dada wanne:
Angela, Juanita, Emma na Agustina. Mke wa kwanza wa Castro alikuwa akijulikana
kama Angel, lakini akaja kumpata Maria Argota, ambaye alimzalia watoto wengine
watano wa Raúl: Pedro Emilio, Maria Lidia, Manuel, Antonia na Georgina. Kama
watoto, ndugu wa Castro walifukuzwa kutoka shule ya kwanza waliyokuwa wakisoma.
Kama ilivyokuwa kwa Fidel, Raúl baadaye alikwenda katika Shule ya Yesuit ya Colegio Dolores katika Shule ya Maandalizi ya Santiago na Belen Jesuit huko Havana. Raúl, alipata shahada ya kwanza, katika masomo ya sayansi ya Jamii. Ingawa Fidel alipendelea kuwa mwanafunzi, Raúl aligeukia sanaa za majukwaani katika maonyesho makubwa. Raúl akawa mshirika wa ujamaa na alijiunga na Vijana wa Kijamii, mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha Cuban cha Soviet-oriented, Partido Socialista Popular (PSP).
Wakiwa katika chama hicho akiwa pamoja na kaka yake wakati mwingine walishiriki kikamilifu katika vitendo vya wanafunzi kuleta vurugu. Akiwa katika chama cha kikomunisti Raul alianza kuwasiliana na wakala wa kisovieti KGB Nikolai Leonov ambaye alikutana naye mwaka 1953 na baadaye mwaka 1955 wakati wa uhamisho huko Mexico City.
Kutokana na kufanikisha mapinduzi ya Cuba ilionekana kuwa Leonov angepata kuwa mjumbe wa KGB huko Havana. Mnamo mwaka wa 1953, Raúl alihudumu kama mwanachama wa kikundi cha ‘Julai 26’ ambacho kililishambulia Kambi ya Kijeshi ya Moncada; hiyo ilikuwa kama kisasi baada ya Raul kutupwa jela miezi 22.
Licha ya kwamba mapambano hayo ya mwaka 1953 yalishindwa yakiwa na malengo ya kumuondoa madarakani dikiteta Fulgencio Batista lakini yalichangia kumwingiza madarakani Fidel Castro (kaka yake Raul) ambaye alishika hatamu za kuliongoza taifa ya Cuba mwaka 1959. Waliposhindwa kumwondoa madarakani Batista walitupwa jela hadi mwaka 1955 kwa kitendo hicho. Wakati Fidel Castro alipoingia madarakani Raul alimuoa mwanamapinduzi mwenzake Vilma Espin Guillois.
Kwa miongo mingi Raul alikuwa kiungo muhimu katika taifa la Cuba huku akiungwa mkono na maafisa wakubwa wa jeshi la nchi hiyo ambao ilifikia kuitana ‘raulistas.’ Raul alisalia katika chama cha kikomunisti cha CPC ambacho alikisaidia kiweze kuendelea na kuwa taasisi kamili yenye misingi imara.
Hakuishia hapo alizidi kuimarisha mahusiano na Umoja wa Kisovieti ambapo mwaka 1962 alisafiri kwenda katika umoja huo akiwa na ombi la silaha kwa ajili ya majeshi ya nchini Cuba. Licha ya mambo yote Raul alionyesha nia ya dhati ya kufufua sera za uchumi wa taifa hilo tofauti na kaka yake alivyokuwa akifanya.
Miaka ya katika ya 1980 aliruhusu majeshi ya Cuba kufanya mabadiliko katika baadhi ya taasisi zilizokuwa zikimilikiwa na serikali zipate kumilikiwa na jeshi. Matokeo makubwa ya hatua hiyo yalionekana baada ya anguko la USSR baada ya mfarakano wa kiuchumi ambapo Raul alisaidia kuifufua miradi ya kiuchumi ya Cuba iliyoanguka hadi katikati ya miaka ya 1990. Kwasababu ya kuongoza kwa muda mrefu kama Waziri wa Ulinzi ushawishi wake ulienea hadi kwa mawaziri wengine katika taifa hilo.
Julai 31, 2006 alitangazwa kuwa mrithi wa Fidel Castro ambaye alikuwa mgonjwa baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na maradhi ya utumbo. Akiwa katika nafasi mpya Raul aliahidi kuwa atasuluhisha matatizo ya Cuba chini ya mwavuli wa chama cha Kikomunisti CPC. Septemba 2006 alifanikiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa maraisi wa nchi 50 wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na uliofanyika Havana lakini hakuonyesha ushirikiano mkubwa sana kwani alikuwa katika majadiliano ya kidiplomasia na Marekani kusuluhisha mgogoro wao wa siku nyingi baina yao.
Hata hivyo Raul anasalia kuwa imara katika taifa hilo licha ya kufiwa na mkewe ambaye walipambana naye katika mapinduzi ya kumwingiza kaka yake katika madaraka ya kuliongoza taifa hilo. Mkewe anafahamika nchini Cuba kama FIRST LADY katika mapinduzi ya Cuba.

Baada
ya Fidel kutangazakwamba hataweza kuendelea tena na kipindi kingine katika
nfasi ya uraisi kutokana na matatizo ya kiafya, Raul alichukua hatamu za
kuliongoza taifa hilo licha ya kwamba alitamka hadharani kwamba ataendelea
kuzungumza na kaka yake ili aweze kuendelea kutokana na masuala mbalimbali
ambayo yeye ndiye muhimili mkuu.
Baada ya kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo miezi michache iliyofuata Raul alifanya mabadiliko kadhaa ikiwamo kuondoa vikwazovya mishahara vilivyowekwa tangu miaka ya 1960. Pia Raul aliruhusu matumizi ya simu za viganjani na kompyuta kiwa raia wa taifa hilo. Lakini Raul aliruhusu raia wake kuweza kuishi katika hoteli ambazo awali ziliwekwa kwa ajili ya wageni tu kutoka mataifa mengine, na ilikuwa ni kosa kwa raia wa Cuba kukutwa ukikaa hotelini.
Mnamo Septemba 2010 Raul alikwenda mbali zaidi alipotangaza kuongeza wataalamu kutoka sekta binafsi na kwamba waajiriwa wa serikali akali ya 500,000 waliondolewa. Mwaka 2011 alimpokea Fidel Castro kiti cha kuwa Katibu Mkuu wa chma cha Kikomunisti CPC.
Itakumbukwa kwamba Agosti ya mwaka 2011 Raul alianzisha mfumo wa mabadiliko ikiwamo nguvu ya serikali katika sekta muhimu ilipunguzwa huku wafanyakazi wa serikali wakipoteza jira zao. Pia katika mabadiliko hayo ya Raul aliyoyafanya aliondoa vikwazo vya watu kusafiri ndani nan je ya taifa hilo.

Mnamo
mwaka 2012 Raul alitangaza rasmi kuwa watu wote waliosaidia kufanyika kwa
mapinduzi ya taifa hilo wana fursa ya kihistoria ya kusahihisha makosa yao wenyewe
kutokana na vile walivyotenda. Wakati wakielekea katika uchaguzi mwingine wa
taifa hilo Februari 2013 alitangaza kwamba hataweza kuendelea tena na kipindi
kingine baada ya hichokitakapofika mwisho wake mwaka 2018.
Akiwa katika kipindi hicho cha mwisho cha utawala wake Raul alishuhudia kaka yake waliyepambana naye kuiweka Cuba hapo ilipofikia Fidel Castro akipoteza maisha. Fidel alipoteza maisha Novemba 26, 2016 akiwa na umri wa miaka 90. Raul ndiye aliyetangaza kifo hicho
Katika
kipindi hicho chote Raul aliendelea kufanya mabadiliko kadha wa kadha katika
taifa hilo hususani katika matarajio ya muda mfupi katika medani ya uchumi ili
kuweza kufikia malengo ya muda mrefu katika siasa. Aliwasaidia raia wa Cuba
kuchukua makazi ya muda ugenini ili kuweza kujipatia ajira huku taifa hilo
likifaidi mapato kupitia fedha za kigeni.
Akiwa katika kipindi hicho cha mwisho cha utawala wake Raul alishuhudia kaka yake waliyepambana naye kuiweka Cuba hapo ilipofikia Fidel Castro akipoteza maisha. Fidel alipoteza maisha Novemba 26, 2016 akiwa na umri wa miaka 90. Raul ndiye aliyetangaza kifo hicho
Fidel Castro mwaka 1971 |
Uchumi mtambuka katika taifa hilo umesababisha taasisi za ummankutaifishwa kwa watu binafsi. Katika medani ya kisiasa Julai 2013 kulifanyika maadhimisho ya miaka 60 ya kuvamiwa kwa kambi za kijeshi za Moncada, kitendo hicho kiliamsha hisia za Wacuba wengi hususani waliopo katika chama cha Kikomunisti ambao kwa muda mrefu walikuwa na shauku ya kufanya maadhimisho hayo. Katika hotuba yake kwenye maadhimisho hayo Raul alitambua mchango wa raia wa Cuba na kusema asilimia 70 ya idadi ya watu wa Cuba wamezaliwa baada ya mapinduzi hayo.
Kizazi cha Historia katika Cuba cha wanaume na wanawake kilichoshiriki kuuondoa utawala dhalimu wa dikteta Batista mwaka 1959 kilikuwa kimejivika ujasiri kwa kunyanyua mabango yalioandikwa Mapinduzi na Ujamaa.
Miongoni
mwa waliozaliwa ni Rais wa sasa wa Cuba Miguel Diaz-Canel ambaye awali alipokea
kiti cha Makamu wa Rais Jose Ramon Machado Ventura kabla ya kuchukua kwa Raul.
Tukio
kubwa ambalo halitasahulika ni lile la Desemba 2013 ambapo Raul alishikana
mikono na Rais wa Marekani wakati huo Barrack Obama katika maziko ya kiongozi
shupavu wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Kitendo hicho kilionyesha wazi kuwa uhusiano baina ya Cuba na Marekani umeanza kurudi. Miezi 18 baadaye Obama aliushangaza ulimwengu makubaliano ya siri yaliyosimamiwa na Canada na Vatican kwamba uhusiano baina ya Cuba na Marekani uliovurugika tangu Januari 1961 utarudi katika hali yake. Viongozi wote walijitokeza mbele ya televisheni na kutangaza licha ya Raul kusisitiza kuwa kuna haja ya Marekani kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Cuba.

Julai
2015 ikiwa ni baada ya miaka 50 ya migongano ya mataifa hayo yalifikia alama
muhimu ya kuzifungua tena balozi za mataifa yao.
Machi 2016 kwa msisitizo mkubwa Obama
alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuzuru taifa hilo ikiwa
ni miaka miaka 88 kwa kiongozi wa Marekani kufanya hivyo. Katika
makubaliano yao ya kidiplomasia walikubaliana kulegeza vikwazo vya kusafiri na
vaya kiuchumi.
Wengi walitoa mitazamo yao tofauti kwamba ziara ya Obama katika taifa hilo huenda ukawa kikwazo kikubwa cha mbadiliko makubwa ya kiuchumi ambayo taifa hilo yamefanya kupitia kiongozi wao Raul. Katika hotuba yake kwa Wacuba na chama cha Kikomunisti CPC Raul mwezi mmoja baadaye aliwaambia kuwa hakufanya haraka kufanya mabadiliko bali alienda hatua kwa hatua.
Aprili 19, 2018 aliachia rasmi kiti cha uraisi na nafasi yake ikachukuliwa na Miguel Diaz-Canel.

0 Comments:
Post a Comment