Wednesday, June 5, 2019

Ashira yapokea magodoro ya msaada


Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Kilimanjaro, wamekabidhi jumla ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 4.2 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Ashira, iliyopo Marangu mkoani humo  ambayo iliungua Mei 23 mwaka huu. 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi, amesema baada ya kusikia tukio hilo wameguswa hivyo wameona haja kuwapa pole kwa ajili ya janga hilo. 


Kwa kuanza CCM imetoa  magodoro hayo 65 ambayo yametokana na msaada kutoka kwa wadau mbalimbali, walioguswa na kuwaunga mkono watoto hao. 

Aidha Mwenyekitti huyo wa CCM  amewataka  wanafunzi hao kusoma kwa bidii, na kuacha tabia ya  kutumia muda wao vibaya, bali wautumie kwa kujisomea zaidi. 

Kwa upande wake Mkuu  wa shule hiyo Madam  Elizabeth Abdallah, amesema tayari wahandisi wameshafika katika shule hiyo ili kufanya tathmini ya shule kwa ajili ya kuifanyia ukarabati ambapo mabweni mawili yaliungua.

0 Comments:

Post a Comment