Thursday, July 14, 2022

RC Kigaigai athibitisha ujio wa Makamu wa Rais Dkt. Mpango

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kigaigai

 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kigaigai amethibitisha ujio wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anayetarajiwa kuingia Julai 15, 2022.

Kigaigai amesema Makamu wa Rais atafanya ziara ya siku tatu mkoani humo hadi Julai 18, ambapo atafungua Maabara ya Kisasa katika Hospitali ya Kibong’oto na Hospitali ya Wilaya ya Rombo.

Kigaigai alianza kuuongoza mkoa huo tangu Mei 15, 2021 akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Dkt. Anna Mghwira aliongoza mkoa huo tangu Juni 3, 2017 hadi Mei 15, 2021.

Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

0 Comments:

Post a Comment