Afisa Ustawi wa Jamii Ally Shehoza amesema moja ya sababu inayowafanya wanawake kupandikiza mbegu za uzazi ni kutowajibika kwa wababa kwenye malezi na matunzo ya mtoto.
“Wanawake wengi wamekuwa wanafikiria kufanya matukio hayo ya kupandikiza mbegu kwa sababu ya kutowajibika kwa wababa, kwa hiyo anaona ni bora asiwe na mtu wa kumtegemea wa kumtunza mtoto," amesema Shehoza
Hata hivyo Afisa Ustawi huyo amesisitiza kuwa licha ya kila mmoja kuwa na haki zake za kimsingi lakini hawashauri mwanamke kufikia hatua hiyo ili kuepusha changamoto zitakazojitokeza siku za usoni.
"Hatu-entertain sana watu wafanye hivyo kwa kupandikiza mbegu kwa sababu ya kuhofia kutotuzwa kama sheria zipo za kumsimamia mtoto. Kuzaliwa na wazazi wake wote wawili ni muhimu zaidi".
Ally Shehoza amesema hivyo baada ya taarifa ya msanii Malkia Karen kusema mtoto wake hana baba na alipandikiza mbegu za uzazi kumpata mtoto huyo.
CHANZO: EATV
0 Comments:
Post a Comment