Profesa George Wajackoyah |
Wajackoyah
anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots.
Alihudumu
kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa
marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka
kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
Yeye ni
mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
Alifundisha
somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
Ahadi zake
endapo atapita kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya
Kuhalalisha
matumizi ya kiviwanda ya bangi, Kubadilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi na kutoa huduma ya afya ya bure na msaada kwa
wazee, walio hatarini na wajawazito.
0 Comments:
Post a Comment