Tuesday, July 19, 2022

Wizara ya Ardhi yafanikiwa kutatua migogoro ya ardhi Siha

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwan Kikwete, amesema  Wizara hiyo imepiga hatua ya kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa imedumo kwa zaidi ya miaka 50  Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro pamoja na kutoa ushauri juu ya matumizi bora ya ardhi.

Kauli hiyo aliitoa Julai 16,2022 mbele ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, wakati alipokaribishwa kutoa salamu za Wizara katika hafla fupi ya ufunguzi wa Maabara ya bAfya ya Jamii ngazi ya Tatu ya Usalama wa Kibailojia ya Kibong;oto iliyofanyika katika viwanja vya hospitali hiyo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

 

Amesema Wizara imeendelea kutekeleza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoiahidi ya kutoa maeneo kwenye vijiji vitatu vya Changare, Ndemeti na Miti Mirefu, vilivyopo Wilaya ya Siha huku akiwataka wananchi wa vijiji hivyo kuanzisha ushirika ambao utasimamia maeneo hayo.

 

“Katika wilaya ya Siha kulikuwa na migogoro mitatu ya ardhi ambayo ilikuwa ikisumbua sana, katika eneo la shamba la Kiraru, kulikuwa na mgogoro baina ya masisita na wananchi, yako mambo ya msingi ambayo sisi kama Wizara ya Ardhi tumeshayafanya, moja ni kuwapatia eka 300 masisita  ili kuweza kuoindoa mgogoro kwa kugomea ardhi na wananchi,”alisema.

Aidha Kikwete amesema Rais Samia ameridhia kusamehe riba ya kodi ya pango la ardhi  kwa wadaiwa sugu  kwa masharti kwamba wadaiwa hao wawe wamelipa madeni yao ndani ya miezi sita kuanzia Julai hadi Desemba mwaka huu.

  

Alisema  mwekezaji huyo amlifikia uamuzi wa kulirudisha eneo hilo serikalini, kutokana na deni hilo kuwa kubwa na Sheria inatukataza kupokea ardhi ambazo zina madeni jambo hilo limeshindwa kuendelea, nipende kukuhakikishia Mbunge Tadayo kwa niaba ya wana Kilimanjaro wote madeni yale Rais Samia ameyasamehe kwa kuondoa riba,”alisema Kikwete.

 

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Kikwete, alisema mmiliki wa ardhi atakaye shindwa kulipa madeni yake katika kipindi cha miezi hiyo sita iliyotolewa  basi atadaiwa madeni yake pamoja na riba.

 

“Rais  Samia ameelekeza msahama huo ni ndani ya miezi sita tu, baada ya miezi hiyo kumalizika kama ulikuwa ukidaiwa milioni 200 utailipa pesa hiyo pamoja na riba yake na akishindwa kufanya hivyo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ambako huko uamuzi wake ni kulipa au kunyang’anywa ardhi anayoimiliki,”alisema.

 

Aliongeza “Wale ambao walikuwa wanadaiwa shilingi milioni moja ambao sasa wanajikuta wakidaiwa shilingi laki nane, ninawaomba kukimbia haraka katika ofisi za ardhi kwa ajili ya kulipia madeni hayo,”.

 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwataka maafisa ardhi kote nchini kuhakikisha kwamba maeneo yote ya taasisi za umma, yanayotoa huduma kwa wananchi zikiwemo shule, hospitali  yanapimwa ili kuondoa uvamizi.

0 Comments:

Post a Comment